Msanii wa filamu Bongo, Wastara Juma amefunguka kuwa tangu mume wake
Juma Kilowoko ‘Sajuki’ afariki dunia, wamekuwa wakijitokeza wanaume
kibao wakitaka kumuoa lakini amegundua wengi wana nia ya kunitumia tu.
Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Wastara alisema kama
mwanamke amekuwa akitamani kumpata mwanaume wa kumfariji lakini
kinachomchanganya ni sampuli ya wanaume wanaotuma maombi kwake.
“Mpaka sasa wameshanitokea wanaume zaidi ya kumi lakini wengi wao
nawaona wananitaka ili kujua nini nilichonacho na wengine wananifuata
wakidhani watapata mali na si mapenzi ya dhati.
“Kimsingi wanataka tu kujua Sajuki alidata na nini kwangu, mimi siko
hivyo. Siwezi kumruhusu mtu aingie kwenye maisha yangu kwa masilahi
yake. Ninayemhitaji namjua moyoni na ipo siku nitampata kwani siangalii
mfuko wa mtu, naangalia tabia,” alisema Wastara.