MUUZA sura wa sinema za Kibongo, Salma Salmini
‘Sandra’ ametoa dukuduku lake baada ya kuelezea mateso aliyopata kipindi
alipokuwa anaanza kujihusisha na masuala ya sanaa katika Kundi la
Kaole.
Sandra aliliambia Ijumaa kuwa, mateso anayoyazungumzia ni yale ya
kunyanyaswa na wasanii wenzake huku wakimfanyia vitimbi vya kila aina
ili asifikie malengo yake lakini anamshukuru Mungu aliweza kuhimili.
“Kila nikikumbuka roho inaniuma maana kuna watu walikuwa na chuki na
mimi za waziwazi, walitamani wanitoe roho. Kusema kweli niliteseka mno
mpaka kupata nafasi ya kuanza kuonekana kwenye runinga na kufikia hapa
nilipo,” alisema Sandra.