Search in This Blog

Showing posts with label KAJALA. Show all posts
Showing posts with label KAJALA. Show all posts

KAJALA: WEMA NI MNAFIKI NA PIA NI KIGEUGEU


Musa Mateja na Shakoor Jongo STAA wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja ameibuka na kusema kuwa ushosti wake na Miss Tanzania 2006/07, Wema Sepetu, uliorudishwa hivi karibuni baada ya kuwekana sawa ni wa kinafiki huku akidai Wema ni kigeugeu.
Staa wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja
Akizungumza kwa kujiamini mbele ya waandishi wetu, juzi Jumatano pande wa Mikocheni jijini Dar es Salaam, Kajala alisema: “Wema ni mnafiki kabisa. Upatanisho wetu ni wa uongo. Mimi moyoni nimeondoa kinyongo lakini mwenzangu naona kama bado ana donge moyoni.”
Kajala alisema hayo alipoulizwa na Risasi Jumamosi, sababu ya kutoonekana kwenye tukio la futari lililofanyika nyumbani kwa mama mzazi wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sanura Kassim ambaye ni mkwe wa shosti wake huyo.
Katika tukio hilo, mama Diamond alifanyiwa sapraizi ya nguvu alipokabidhiwa gari kali aina ya Toyota Lexus Harrier kama zawadi ya bethidei yake, ambayo ilitolewa na meneja wa Diamond, Babu Tale kwa niaba ya mwanamuziki huyo ambaye alikuwa safarini nchini Marekani.
Miss Tanzania 2006/07, Wema Sepetu,
“Tunakubaliana kuwa kitu kimoja lakini mwenzangu anaonekana ana kinyongo. Hebu angalia, anawezaje kuacha kunialika kwenye shughuli muhimu kama ile kama kweli tumepatana? Mbona amealika watu wengi lakini mimi ameniacha? Wema aache unafiki bwana.
“Mbaya zaidi, hivi juzi tu ameweka picha ya msichana mmoja anayekaa China, huyu mdada anaitwa Sabrina, niliwahi kugomabana naye, lakini yeye amemuweka Instagram na kumwandikia maneno kibao ya kumsifia akim-wish happy birthday, hapo si kama ananisimanga? Wema si mkweli,” alisema Kajala.
Akizungumzia ishu hiyo, siku ya tukio Wema alisema: “Ukiniuliza kuhusu Kajala kutokuwepo hapa, kwa kweli utakuwa kama unanichanganya tu maana leo sijashika simu muda mrefu sana.
“Hata ujio wangu hapa nilikurupushwa, ndiyo maana sijakumbuka kumuita Kajala, lakini tuko vizuri na mara ya mwisho tumeongea jana (Jumapili) usiku tu,” alisema Wema.

KAJALA AJIGAMBA KUKAA DAWATI MOJA NA MTOTO WA RAISI KIKWETE

Na Imelda Mtema
HII ni safu mpya ambayo itakuwa ikizungumzia juu ya maisha ya kweli ya mtu yeyote maarufu. Itatokana na mahojiano ya ana kwa ana!

Kwa kuanzia, tunaye nyota wa filamu za hapa nyumbani, Kajala Masanja, ambaye kabla ya kujiingiza kwenye sanaa hiyo aliwahi kuishi kinyumba na mmiliki wa studio ya Bongo Records, Paul Matheas, maarufu kama P.Funk na kujaaliwa kupata mtoto mmoja aitwaye Paula.
Katika safu hii, Kajala ambaye amewahi kukutwa na misukosuko lukuki ikiwemo kuhukumiwa kifungo jela, anaelezea mambo mengi kuhusiana na maisha yake ambayo hakuwahi kuyaelezea kokote kule au katika chombo chochote cha habari.
“Nilizaliwa mwaka 1983 katika familia ya mzee Masanja na walijaaliwa kuwa na watoto wawili tu, mimi na mdogo wangu, Dorice. Sisi tuna tofauti kubwa sana ya umri kati yetu kwa vile tulipishana sana kuzaliwa. Wakati nikizaliwa, wazazi wangu ambao wote ni askari polisi, walikuwa wakifanya kazi na kuishi kituo cha Oysterbay jijini Dar es Salaam.
“Kutokana na kukaa muda mrefu utotoni nikiwa peke yangu, matokeo yake nilijikuta nikiishi kwa kudekezwa sana. Nilipofikisha umri wa miaka sita, nilipata shauku ya kuanza shule kwani nilikuwa nafurahi sana kuwaona watoto wenzangu wakipita pale wakienda na kurudi shuleni.
“Baada ya kuandikishwa Shule ya Msingi Mbuyuni, siku ya kwanza niliyotakiwa kwenda niliamka asubuhi na mapema na dada aliyekuwa akinilea alinivalisha nguo za shule na kunitaka sasa kusubiri chai kabla ya kunipeleka shuleni.
“Wakati dada akiipua chai ili animiminie kwenye kikombe, kwa bahati mbaya ilinimwagikia mapajani na kuniunguza sehemu kubwa ya mapaja yangu. Ikabidi wazazi wangu wafuatwe kituoni hasa kwa kuwa hakukuwa mbali na nyumbani, ambao walifika na kunipeleka hospitalini. Ndoto ya kusoma ikaishia hapohapo!
“Nilipofika hospitali, walinipa dawa na kila siku nilikuwa nikienda kuosha kidonda, hamu ya shule ikaniishia, nikawa mtu wa kulala tu, maana hata kutembea nilikuwa siwezi, kwani nilipohitaji kutembea nilibebwa na kufanyiwa kila kitu hadi nilipopata nafuu.
“Hali yangu iliendelea kuimarika hadi nilipopona kabisa na kuanza kwenda shuleni, ambako nilikutana na watoto wenzangu ambao tukajikuta tukijenga urafiki. Nilikuwa mpole mno, sikuwa mtu wa kuongea kabisa na mara nyingi watoto wenzangu wakorofi walipenda sana kunichokoza.
“Wakati huo nikisoma, mwalimu wangu wa darasa alikuwa Mama Salma Kikwete ambaye sasa ni first lady na nilikaa dawati moja na watoto wa Rais Kikwete, Ridhiwan na Miraji na kwa kweli walikuwa ni marafiki zangu wakubwa sana.
“Nakumbuka nilipofika darasa la sita, kuna msichana mmoja alipanga kunipiga yeye na marafiki zake kwa madai kuwa mimi nimemchukulia mchumba wake, maana kipindi hicho ni wadogo na kutokana na upole wangu niliwaambia mimi sijafanya hivyo wakaniambia kesho yake lazima wanipige, maana enzi hizo tukitaka kupigana, lazima iwe Ijumaa.
“Siku hiyo ilipofika, mama alikuja kuniamsha asubuhi kwa ajili ya kwenda shuleni, nikajifanya nimebanwa na tumbo, siwezi kuamka wala kutembea, akanitafutia dawa na kunipa ninywe kisha akaniambia nilale. Nilishukuru sana kwani siku hiyo niliepuka kipigo.
“Ilipofika Jumatatu nikaendelea na mambo yangu kama kawaida wala hawakunisemesha tena, lakini nilikuwa muoga sana, nilijua wakati wowote wanaweza kunivizia na kunipiga, lakini haikutokea ingawa hata mimi rafiki zangu walikuwa wamejipanga kwa ajili ya kujibu mashambulizi.
“Niliendelea kusoma shuleni hapo kwa amani mpaka nilipomaliza darasa la saba. Wakati huo nilikuwa na rafiki yangu mmoja wa kiume ambaye kila siku jioni alikuwa akipita nyumbani. Baba yangu akamshtukia, siku moja alichukua manati yake aliyokuwa akiitumia kuwapigia kunguru, alipopita akampiga nayo!
“Kufuatia kitendo hicho, rafiki yangu yule hakupita tena nyumbani na akatokea kunichukia sana kwa ajili ya kitendo alichofanyiwa, wakati wa kuanza sekondari ulipofika, nilipelekwa Songea katika shule ya masista kwa hofu kuwa nikisoma mjini nitaharibika kimaadili.
“Nilipoanza masomo shuleni hapo, nilikuwa mpweke sana maana sikuwahi kukaa mbali na wazazi wangu, halafu kulikuwa na baridi sana kitendo kilichosababisha nisiwe naoga kabisa na kujikuta nikipata ukurutu kwa uoga wa kuoga maji ya baridi.”
ENDELEA kufuatilia kila Jumatatu katika gazeti hili kuhusiana na maisha ya Kajala yaliyo na misukosuko inayotisha na kusikitisha.

"VIYOYOZI VYA KICHINA NI VIZURI KULIKO VYA BONGO, HUONI VIMENIBADILISHA" HAYA NI MANENO YA KAJALA

MWIGIZAJI Kajala Masanja amekanusha vikali suala la kujipodoa badala yake amesema kiyoyozi cha nchini China kimeifanya ngozi yake ibadilike.
Kajala Masanja.
Akizungumza na paparazi wetu mwishoni mwa wiki iliyopita, Kajala akiwa katika harakati za kuelekea China alisema amekuwa akiipenda nchi hiyo kwani akiwa huko ni ‘full’ kiyoyozi ambacho kimemfanya aonekane mweupe.
“Ngozi yangu inabadilika na kuwa nzuri sana, China kunanipenda. Kiyoyozi mwanzo mwisho lazima uwe mweupe,” alisema mwigizaji huyo.

WAFUNGWA WATUMA KEKI BIRTHDAY YA KAJALA


Keki iliyotumwa na wafungwa katika ‘bethidei’ ya Mwigizaji Kajala Masanja.
Na Imelda Mtema
KATIKA hali ya kushangaza, baadhi ya wafungwa walio nyuma ya nondo za Gereza la Segerea a.k.a Segedansi, Dar, wametuma keki ya ‘bethidei’ kwa Mwigizaji Kajala Masanja ikiwa ni miezi michache tangu alipoachiwa huru baada ya Wema Isaac Sepetu kumlipia faini ya Sh. milioni 13.

Kajala akishika sahani ya keki kwa ajili ya kumlisha Wema.
Tukio hilo lilijiri Jumatatu iliyopita Julai 22, mwaka huu ambapo mwanadashosti huyo alikuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa bila kutaja umri aliofikisha.
Kabla ya pati hiyo na zoezi la kukata keki ikiwemo iliyotumwa na wafungwa hao, iliyopangwa kufanyika wakati wa kufuturu, Kajala aliianza siku hiyo kwa kwenda kutoa misaada kwa watoto yatima.

Baadhi ya keki alizoletewa Kajala.
Huku akiongozana na rafiki zake, Kajala alikata keki yake ya  kwanza katika Kituo cha Watoto Yatima cha  Mitindo House Talent (MHT), kilichopo Msasani, Dar, kinachomilikiwa na  mbunifu maarufu wa mavazi, Khadija Mwanamboka.
Baada ya kukata keki mbili ambazo alikwenda nazo kituoni hapo, Kajala pamoja na wapambe aliongozana nao walikwenda moja kwa moja nyumbani kwa Beautiful Onyinye au Madam Wema, Kijitonyama jijini Dar ambapo shughuli nzima ilichukua nafasi wakati wa futari.
Katika futari hiyo ambayo ilikuwa ni kwa ajili ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya Kajala, walialikwa watu mbalimbali huku kukiwa na vyakula vya kila aina wakiwemo mbuzi wawili wa kuchoma.
Baada ya futari watu walihamia kwenye ukataji wa keki zilizokuwa mezani zipatazo kumi na tano kutoka kwa marafiki wa Kajala huku Wema akiwa amenunua keki tano kwa ajili ya ‘shostito’, wake huyo.
Katika keki zote, iliyowafurahisha watu wengi ni ile iliyotumwa na wafungwa wa Gereza la Segerea iliyokuwa imeandikwa ‘Happy Birthday Mkuu wa Nyapara From Segerea Crew 2013’ ambayo kila mtu aliyeisoma alikuwa akicheka na kuanza kumtania mwanadada huyo kuwa ni Nyapara.
Kajala alisema kuwa Keki hiyo kutoka ilimkumbusha maisha ya gerezani lakini pia alifurahi kuona watu aliokuwa nao lupango humo  kumkumbuka hivyo alifarijika kupita maelezo.
Kajala alitupwa gerezani wakati kesi yake na mumewe Faraji Agustino ya kutakatisha fedha haramu ikiunguruma ambapo baada ya hukumu, mwanadada huyo alitakiwa kwenda jela miaka mitano lakini alilipiwa faini na kurejea uraiani huku mumewe akienda ndani.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger