MWIGIZAJI Kajala Masanja amekanusha vikali suala la kujipodoa badala
yake amesema kiyoyozi cha nchini China kimeifanya ngozi yake ibadilike.
Akizungumza na paparazi wetu mwishoni mwa wiki iliyopita, Kajala
akiwa katika harakati za kuelekea China alisema amekuwa akiipenda nchi
hiyo kwani akiwa huko ni ‘full’ kiyoyozi ambacho kimemfanya aonekane
mweupe.
“Ngozi
yangu inabadilika na kuwa nzuri sana, China kunanipenda. Kiyoyozi
mwanzo mwisho lazima uwe mweupe,” alisema mwigizaji huyo.