MWIGIZAJI mkongwe Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’ amesema anaamini kwa dalili alizoanza kuziona, mwaka huu utakuwa ni wa faraja kwake.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni juu ya dira ya mwaka 2014,
Mainda alisema mwaka jana aliamua kuokoka baada ya kubaini kuna mambo
anamkosea Mungu na imani yake ni kwamba Mungu atamsamehe na kumfungulia
milango ya neema.
“Nimegundua
wapi nilikosea na kwa kuwa nimeamua kumuabudu Mungu kikamilifu, naamini
kila kitu kitakuwa sawa. Nimeingia kwenye wokovu nikiwa kama mtoto
mchanga, naendelea kukomaa.
Yapo ambayo nilikosea kama vile kutumia mkorogo lakini mwaka mpya na mambo mapya,” alisema Mainda.