UA zuri kunako anga la sinema Bongo, Shamsa Ford amejikuta akipoteza
utulivu kikaoni kufuatia kuinuka na kuzama toileti mara kwa mara.
Tukio hilo lilichukua nafasi hivi karibuni kwenye kikao cha mdahalo
wa kugombea nafasi za viongozi wapya wa Klabu ya Bongo Movies katika
Viwanja vya Leaders Club jijini Dar.
Tathmini za paparazi wetu, Shamsa aliyeonekana akipiga mtungi kiaina,
zilibaini kuwa staa huyo aliinuka kwenda toileti zaidi ya mara sita
hivyo kufanya watu wapoteze utulivu kwa kumuangalia.
“Mh! Hii kali sasa, bora angesubiri kikao kiishe ndiyo apige mtungi
sasa hapa anatibua hali ya hewa,” alisikika mwigizaji mmoja mkubwa.