Mwalimu mmoja wa kike mwenye miaka 35 anatuhumiwa kufanya mapenzi na wanafunzi wake wawili wenye umri chini ya miaka 18 nyumbani kwake, ndani ya gari lake na bustanini.
Mwalimu huyo Jamila Love Williams, anayetokea Michigan, anadaiwa kukiri mahusiano hayo ya kimapenzi na alitarajiwa kurejeshwa katika gereza la Kent County wakati wowote jana.
Waendesha mashitaka walithibitisha hati dhidi yake kwa makosa manne ya kujihusisha na vitendo vya ngono, kosa ambalo adhabu yake ni kifungo cha hadi kufikia miaka 15.
Kwa mujibu wa nyaraka za mahakama, mvulana mmoja mwenye miaka 16 aliwaeleza wapelelezi kwamba alikuwa katika darasa la Jamila na alifanya naye mapenzi mara kadhaa nyumbani kwake, ndani ya gari lake, kwenye bustani na maeneo mbalimbali.
Mwanafunzi mwingine katika darasa lake, mwenye umri wa miaka 15, aliwaeleza polisi alikutana na mwalimu wake nyuma ya nyumba yao kwenye kichochoro na pia alifanya naye mapenzi ndani ya gari lake, kwa mujibu wa ripoti.
Wapelelezi wa polisi wa Grand Rapids walianzisha uchunguzi baada ya wazazi kadhaa na wanafunzi kupeleka madai kwa viongozi wa shule Jumatatu.
Jamila alikiri kwamba alikuwa akifanya mapenzi na wavulana hao wawili, kwa mujibu wa nyaraka za mahakama.
Kwa sasa amepewa likizo ya lazima.