Search in This Blog

WATANGAZAJI WA RADIO CLOUDS FM SASA WALINDWA NA MABAUNSA MAALUM, MASHABIKI WAFUNGUKA!

Watangazaji wa Radio Clouds Fm waliovaa tisheti nyeupe Kulia ni Mirrad Ayo na katikati ni B 12 wakilindwa na baunsa maalum, Ilikuwa kwenye uwanja wa Jamhuri wiki iliyopita wakati wa kutoa Last Respect kwa mwanamuziki Arbeth Mangwair.
M
B12 akiwa amemshika nyoga mtoto mkali ambae hakufahamika jina lake hivi karibuni.




Mirrad Ayo akiwa kwenye moja ya shughuri zake za utangazaji kuripoti matukio, Lakini kwa sasa hali imekuwa tofauti kwa mtangazaji huyo ambae hawezi kujichanganya sehemu yoyote yenye mkusanyiko wa mashabiki bila kuwa na ulinzi wa mabaunsa.Hali inazusha minong'ono mingi kwa mshabiki.


Na Livingstone Mkoi, Morogoro
Katika hali isiyokuwa ya kawaida na kushangaza watangazaji wa kituo cha radio Cluod Fm cha Jijini Dar wiki iliyopita waliwaacha watu midomo wazi kwa hatua ya mtindo wa kutembea na mabaunsa maalum wa kuwalinda wakati hawakuwa na utamaduni huo toka awali.
Mwandishi wetu aliyekuwa ndani ya viwanja hivyo alishuhudia watangazaji hao Mirrad Ayo na B 12 wakiwa chini ya usalama mkali wa mabaunsa hao na kusababisha kuzua minong'ong'ono kibao kwa mashabiki huku wengine wakihusisha sababu za kujiwekea ulinzi ni kutokana na mabifu yaliyopo sasa kati ya baadhi ya wanamuziki na uongozi wa kituo hicho namba moja cha burudani Afrika Mashariki na kati.
Mashabiki wengi waliendelea kujiuliza kulikoni na kusema watangazaji hao awali walikuwa vipenzi kwa mashabiki wa burudani lakini kwa sasa hali imebadilika ambapo watangazaji hao hawana amani ya maisha yao hata kidogo huku wakijiwekea tahadhari ya usalama wao kila wanapojichanganya kwenye viunga vya burudani.

Hata hivyo mmoja wa mashabiki wa muziki wa kizazi kipya mkoani humo aliyejitambulisha kwa jina la Mkude alisema "Matokea haya ya watangazaji kutembea na walinzi wakati hawakuwa na kawaida hiyo awali ni matokeo mabaya sana na inaonesha dhahiri kuwa hata mshabiki hawafurahishi kusikia kituo hicho kikiingia kwenye migogoro na wanamuziki ambao kimsingi wananguvu kubwa sana kwenye jamii kuliko  chombo chochote cha media" Alisema kijana huyo.

Aidha nae mdau wa muziki wa kizazi kipya Mkoani Morogoro na Katibu Tarafa  Uranga na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa taifa CCM Maliki Marupu ambae aliongea na mwandishi wetu alisema kuwa ni vyema uongozi wa radio hiyo ukakaa chini na kutafarakari kuondoa tofauti zilizopo kati yao na wanamuziki ili kurudisha imani yao kwa mshabiki ambao kwa sasa wameghathirika kutokana na utofauti huo
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger