POLISI wa kike wa Kituo cha
Magomeni, jijini Dar es Salaam aliyejulikana kwa jina moja la Anisa,
ametimuliwa kazi kwa madai ya kupiga picha ya utupu iliyosambaa
mitandaoni.
“Anisa aliitwa makao makuu, mabosi wakamuonesha picha yake akiwa mtupu kitandani, akakiri ni yeye. Alijitetea eti alifanya hivyo kwa sababu siku ya tukio alikuwa amelewa sana,” kilisema chanzo.
Chanzo kiliendelea kudai kwamba baada ya afande huyo mwenyeji wa Tanga kukiri, viongozi wa jeshi hilo walimwambia amekiuka kanuni na kulidhalilisha jeshi hilo hivyo hataendelea kuwa mtumishi.Picha ya afande huyo imeenea mitandaoni na kwenye baadhi ya simu za mikononi za watu kitendo kulicholifanya jeshi hilo kufanya uchunguzi na kubaini kuwa ni yake.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina, Suleiman Kova alipoulizwa juzi alikiri kufukuzwa kwa askari huyo na kumtaka mwandishi wetu kufuatilia zaidi kwa Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Camilius Wambura ambaye naye alipoulizwa kuhusu tukio hilo alikiri.
‘‘Tunahitaji askari wenye maadili mema ndani ya jeshi letu, yule atakayefanya mambo bila kufuata kanuni na sheria hatua kali zitachukuliwa dhidi yake. Askari muda wote anatakiwa awe mfano bora kwa jamii,’’ alisema Afande Wambura.
Taarifa zaidi zinadai kwamba kwa sasa Anisa anaishi uraiani kama raia wa kawaida