Search in This Blog

Showing posts with label LULU. Show all posts
Showing posts with label LULU. Show all posts

RAY AJIFANYA KUONA AIBU KUMBUSU LULU, AOGOPA YASIJE KUJIRUDIA NA MAREHEMU KANUMBA

STAA wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ amesema alipata wakati mgumu kumpanga mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ kwenye filamu yake ambayo walipaswa kucheza kama wapenzi kwa kuhofia kumbusu.
Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Akizungumza katika kituo kimoja cha runinga cha jijini Dar hivi karibuni, Ray alisema licha ya kuwa Lulu alikuwa anastahili kuigiza katika sinema ya Woman Principle miaka kadhaa iliyopita, aliona Lulu anafaa kutokana na umakini wake lakini akaona bora amchukue Miss Tanzania namba 3, 2003, Nargis Mohammed kwa kuhofia kupata aibu ya kuoneshana malavidavi na Lulu.
 
Vincent Kigosi ‘Ray’.
“Lulu alikuwa na uwezo wa kumudu kipengele hicho, kipindi hicho alikuwa mdogo sana, niliona ni jambo la aibu kidogo kumbusu mdomoni mtoto mdogo kama yeye halafu ni kitu ambacho jamii itakaa ikitazame nikaona bora nimchukue Nagris, Lulu nikampa sini nyingine,” alisema Ray.
Aliongeza kuwa, kikubwa kilichomfanya avutiwe kucheza na Nagris ni kwa sababu ni mwanamke ambaye katulia na hana skendo hivyo itamuongezea heshima na mvuto wa kazi yake katika jamii.

LULU: KAMA KUENDA KUKAA JELA YANGENIKUTA MAZITO


SURA ya mauzo katika sinema za Kibongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ ametoa ya moyoni kuwa kama siyo kuwekwa nyuma ya nondo za Mahabusu ya Segerea, Dar basi yangemkuta mazito.

Lulu alikaa Gereza la Segerea kwa takribani miezi kumi baada ya kutokea kifo cha aliyekuwa mwandani wake, marehemu Steven Kanumba ‘The Great’ aliyefariki dunia Aprili 7, 2012.
Nyota huyo wa Filamu ya Foolish Age alifunguka mambo ya kushangaza hivi karibuni juu ya tukio hilo kupitia Kipindi cha Take-One, kinachorushwa  na Clouds TV.

TATIZO FOOLISH AGE
Lulu alikuwa akizungumzia filamu yake hiyo ya Foolish Age ambapo alisema sinema hiyo inawasihi wasichana ambao wanapitia kipindi cha balehe ambacho ni hatari sana kwao.
“Kwa kweli kipindi cha foolish age ni cha hatari sana, nilicheza filamu hiyo ili kuwaasa wasichana wenzangu.
“Asikwambie mtu, mimi mwenyewe nilikokuwa nikielekea si kuzuri kabisa.

KAMA SIYO KANUMBA
“Ukweli ni kwamba kama siyo matatizo (kifo cha Kanumba) nikaenda mahabusu sijui ingekuwaje sasa hivi. Kukaa jela kulinisaidia kusitisha kasi ya tabia yangu, nikatoka nikiwa mpya.
“Yangenikuta mazito zaidi maana kipindi kile ilikuwa hatari tupu,” alisema Lulu ambaye ni mrembo wa haja.

Staa huyo aliongeza kuwa kipindi hicho kilikuwa cha hatari na hakitamani kijirudie hata kidogo katika maisha yake.
Alisema kwamba si ajabu inawezekana kipindi hicho ndicho kilisababisha matatizo yote yaliyomkuta. Alisema alikuwa akielekea kubaya.

HATAKI KIJIRUDIE
“Ni kipindi ambacho siwezi kukuhitaji tena katika maisha yangu si kizuri na kinatisha maana kuna wakati nilikuwa sisikii la mtu yeyote hata mama yangu mzazi,” alisema Lulu ambaye baada ya kutoka mahabusu haonekani akirandaranda mjini kama zamani.
Kabla ya utulivu huo alioupata nyuma ya nondo, Lulu alikuwa hakauki kwenye kumbi za usiku za starehe huku akilewa tilalila na kuyaweka maisha yake hatarini endapo angefanyiwa kitu mbaya.

Lulu alihusishwa na kifo cha Kanumba kwa kuwa siku ya tukio alidaiwa kuwa naye eneo la tukio ambapo alikamatwa na baadaye kuachiwa kwa dhamana akisubiri kesi ya kuua bila kukusudia.


SKENDO MPYA
Wakati hayo hayajapoa kumeibuka skendo mpya inayomgusa staa huyo mkubwa Bongo.
Madai mazito yameshushwa na wafuatiliaji wa mambo ya watu kuwa nyuma ya mwanadada huyo anayeng’ara kuna mbunge maarufu anayemiliki jimbo kwa kura za wananchi jijini Dar (tutamtaja baadaye).

ILIKUWA HIVI
Sosi: Hivi ninyi Global siku hizi hamuandiki skendo za mastaa?
Global: Tunaandika sana kwani vipi?
Sosi: Mna habari?
Global: Tunazo nyingi fuatilia magazeti yetu lakini ukitupatia ya kwako tutairusha hewani.
Sosi: Sasa mimi nina habari yangu.

Global: Inakuhusu wewe? Funguka. 
Sosi: Hainihusu mimi. Ni ya ‘Kalulu Kadogo’.
Global: Siku hizi amekua, sema Lulu inatosha. Eeh... hiyo habari ikoje?
Sosi: Kwa taarifa yenu siku hizi anatoka na mbunge (anamtaja). Ndiye kamnunulia lile gari analokatiza nalo mjini na kampangishia bonge la mjengo kule Tegeta (Dar). Fuatilieni kwa watu wake wa karibu, naombeni msinitaje.
Global: Hatuwezi kukutaja ngoja tuzame mzigoni.

Gazeti hili lilifanya uchunguzi wake kwa watu wa karibu wa Lulu na kubaini kuwa ni kweli kwa sasa staa huyo amehama Tabata alikokuwa akiishi na mama yake, Lucresia Karugila na kuhamia kwenye bonge la mjengo Tegeta huku akisukuma gari kali (aina haikujulikana mara moja).
Madai mengine yalisema kwamba  mke wa mbunge huyo alishamtafuta Lulu na kumuonya kuachana na mume wake


LULU AFYATUKA  
Baada ya kujiridhisha kuwepo madai hayo, juzi gazeti hili lilimtafuta Lulu na kumsomea mashitaka yake mwanzo hadi mwisho ambapo alifyatuka:
“Hivi ni nani anayeleta habari zangu Global? Analipwa na nani? Maana kila kukicha unasikia hili, halijapoa unasikia lingine.

“Si kweli kwamba natembea na huyo mbunge. Kwanza sina mazoea naye. Nakumbuka nilimuona mara moja tu sikumbuki ilikuwa kwenye shughuli gani.
“Huyo mkewe mimi simjui anafananaje. Nasema huko ni kuchafuana kusikokuwa na maana.”

VIPI KUHUSU KUPANGISHIWA NYUMBA?
“Ni kweli nimehamia Tegeta lakini sijapangishiwa, nimepanga mwenyewe. Hivi nikifanya jambo lazima iwe kuna mwanaume? Watu waache hizo. Wabadilike.”

VIPI KUHUSU GARI?
“Gari ninalo muda mrefu nimenunua kwa fedha yangu. Halina mkono wa mbunge, ni jasho langu.”
Kabla ya kuwekwa mahabusu, Lulu aliwahi kudaiwa kuhongwa nyumba na mbunge mwenye kitambi kikubwa, ishu hiyo aliikanusha kwa nguvu zote.

Imeandikwa na Imelda Mtema na Musa Mateja.
Gpl

" MWENYE SHIDA YA KUNITAFUTA ANITUMIE BARUA, NA KUANZIA HIVI SASA SIHITAJI KUTAFUTWA TENA KWENYE SIMU" LULU

MWANADADA anayetamba katika filamu za Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema kero yake kubwa ni utumiaji wa simu za mkononi na anasumbuliwa sana na watu wasiokuwa na mambo ya msingi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Lulu alisema simu zinasumbua sana na anatamani irudi enzi ya kutumiana barua posta.
“Sitaki kabisa kutumia simu ya mkononi kwa sasa, mwenye shida na mimi atanitumia barua, yaani sijui hata nisimame wapi, kwani hata nikibadili namba ya simu inasambaa kwa kasi sana,” alidai Lulu.

Lulu alibainisha kuwa kwa siku anapigiwa simu zisizo na faida kwake na kwamba, idadi kubwa wanaompigia ni mashabiki wake, lakini wanakuwa na maneno yasiyo na msingi.
“Kwa siku napigiwa simu nyingi sana ambazo ni kero kwangu. Nafurahi sana ninapopigiwa simu na shabiki wangu, lakini wapo wanaopiga simu kutaka mambo ya ajabu, nakubali kwamba wengi wao ni mashabiki wangu, lakini simu kwangu ni kero kubwa, ingawa ni msaada mkubwa pia kwangu kwani ni sehemu ya kitendea kazi,” aliongeza Lulu.

"TANGU NITOKE JELA SIJAWAHI KUKUTANA NA MTU YOYOTE KIMAPENZI HATA SIKU MOJA".....LULU


Elizabeth Michael "Lulu " Amedai hajakutana na mtu yoyote kimapenzi toka atoke Jela ...Kwa mujibu wa chanzo chetu Muigizaji huyo nyota amesema licha ya Vishawishi vingi  vya wanaume na wasagaji lakini hakuna alie bahatika kumnasa mpaka sasa 
Inasemekana toka apatwe na Masahibu ya Kanumba Lulu ni Kama mtu Aliyeng'atwa na Nyoka kwa kuogopa hata kuguswa na Nyasi..
Lulu Ameshabadilisha number mara 13 na tatu kuepukana na Usumbufu

LULU ANALAKE JAMBO MOYONI, KWA NINI APIME MARA LKWA MARA, AU AMEFANYA NA MTU MWENYE UKIMWI , NDO MANA ANAPIMA KILA MARA?

KAULI aliyoitoa msanii nyota wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kuhusu kupima mara kwa mara maambukizi ya ugonjwa hatari wa Ukimwi, imeibua utata mkubwa miongoni mwa wadau wakihoji ana nini moyoni mwake? Amani limeelezwa.
Katika tamasha maalum la Siku ya Ukimwi Duniani lililofanyika Desemba Mosi, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar, Lulu akiwa miongoni mwa waliohudhuria, alikiri kupima virusi vya ugonjwa huo mara kwa mara na kuwataka vijana wengine waige mfano wake.
“Vijana wengi waoga kujitokeza kupima Ukimwi, wanadhani kwa kufanya hivyo ni kujitafutia hofu ya kifo kitu ambacho si kweli.
“Hata mimi nilikuwa muoga sana lakini baada ya kupata elimu stahiki juu ya umuhimu wa kujua afya kila mara, nimekuwa nikipima mara kwa mara, hivyo hata ninyi nawaasa mjenge tabia ya kupima Ukimwi mara kwa mara,” alisema Lulu.

Baadhi ya wadau walihoji kulikoni msanii huyo mwenye historia mbaya huko nyuma, hasa ya starehe awe na tabia hiyo ya kupima Ukimwi mara kwa mara?
Wengi walihoji je amekuwa akipima mara kwa mara kwa sababu huwa anabadilisha wanaume mara kwa mara? Wengine walihoji amekuwa hatumii kinga?
“Kwa nini amekuwa na tabia ya kupima Ukimwi mara kwa mara? Ina maana huwa hatumii kinga? Au ni uaminifu mdogo katika uhusiano?” alihoji mdau mmoja ambaye pia ni msanii mkubwa wa filamu za Kibongo akiomba kusitiriwa jina.
Juzi paparazi wetu alilazimika kumsaka Lulu ili azungumzie kwa kina juu ya mjadala huo lakini simu yake iliita bila kupokelewa.

LULU MICHAEL AANZA KUMTONGOZA JUSTINE BIEBER, ANASEMA HAJAONA MWANAUME MWINGINE YOYOTE ISIPOKUWA YEYE TU

Zikiwa  zimepita  wiki  kadhaa  tangu  Johari  atimkie Canada  kumfuata  mpenzi  wake, Lulu  Michael  naye  ameanza  kujipendekeza  kwa  msanii  Maarufu  Justine  Bieber   kiasi  cha  kudiriki  kumtongoza  mtandaoni...
Kupitia  ukurasa  wake  wa  twitter, Lulu  Michael  amekuwa  akieleza  jinsi  anavyokosa  usingizi  kwa  sababu  ya dume  hilo,  hali  inayomfanya  akonde  na  kukongoroka.

 
Pamoja  na  maneno  mazuri  ya  kumtongoza  mwanaume  huyo, tweet  za  Lulu  zimeonekana  kutokuwa  na  msaada  wowote  kwake  kutokana  na  ukweli  kuwa  Justine  Bieber  ni  mtu  ambaye  hajui  kiswahili...

Mbali  na  kutoijua  lugha  ya  kiswahili, Bieber  ni  mtu  mwenye  followers  wengi  sana  (  47,180,637   followers ), hivyo  ni  ngumu  sana  kutambua  kwamba  kuna  mtu  anayeitwa  Lulu  Michael.


LULU ANGUA KICHEKO OVYO OVYO KWENYE MSIBA WA BABA YAKE WEMA TENA HUKU MISA IKIENDELEA

KATIKA hali isiyotarajiwa, staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amenaswa na kamera yetu akiangua kicheko cha nguvu huku misa ya msiba ikiendelea.
Lulu (wa pili kushoto) akiangua kicheko na shosti wake wakati misa ya msiba ikiendelea.
Tukio hilo lililowaacha midomo wazi waombolezaji lilitokea Jumanne iliyopita nyumbani kwa marehemu baba wa mwigizaji Wema Sepetu ‘Madam’, Isaac Abraham maeneo ya Sinza-Mori, jijini Dar wakati Lulu alipokuwa amekwenda kumfariji mwigizaji mwenzake huyo.
Lulu ambaye alikuwa amevalia sare maalumu waliyovaa watu wa karibu na familia ya marehemu, alinaswa akiwa amejisahau kabisa kama yupo msibani na kuanza kupiga stori na dada mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja.

...Wakizidi kupiga stori na kufurahi wakati wa ibada.
“Mh! Sasa mwenzetu pale amepitiliza haiwezekani ajisahau kiasi kile wakati hapa ni msibani. Atachekaje kiasi kile, hii ni aibu jamani bora hata wangeenda kuchekea pembeni,” alisikika mmoja wa waombolezaji.
Baada ya kugundua papararazi wetu anawafotoa picha, ghafla wawili hao walihamaki na kuacha kucheka huku wakijiziba usoni wasiweze kunaswa sura zao kiurahisi na kamera.
Katikati ya wiki hii, Lulu aliripotiwa kuwa amevurumusha matusi kwa mapaparazi katika msiba huohuo hali ambayo inawafanya mashabiki wahoji kulikoni?

LULU ATOA MITUSI MIZITO KWENYE MSIBA WA BABA WEMA

MSANII nyota wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amejikuta akiporomosha mitusi mizito ya nguoni kwenye msiba wa baba wa Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu, mzee Isaac Abraham Sepetu hali iliyowafanya baadhi ya waombolezaji kumkodolea macho ya mshangao.
Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiwa msibani kwa marehemu Balozi Sepetu.
Tukio hilo lililotawaliwa na hasira lilijiri Oktoba 28, 2013 kwenye msiba huo uliokuwa ukiombolezwa nyumbani kwa marehemu, Sinza-Mori jijini Dar es Salaam.
KISA NA MKASA
Ilikuwa wakati Lulu akitinga msibani hapo, ghafla alimfuata mmoja wa waandishi wa habari hii na kuanza kumporomoshea matusi hayo kwa kile alichodai kukerwa na habari iliyowahi kuandikwa juu ya kitendo chake cha kula chakula sahani tatu katika hafla moja iliyofanyika hivi karibuni huko Kunduchi Beach Hotel, Dar.

TUJIKUMBUSHE KIDOGO
Katika tukio hilo la awali, Lulu alikuwa mmoja wa waalikwa wa harambee ya kuchangia kansa ya matiti kwa akina mama iliyofanyika kwenye hoteli hiyo.

Wakati wa chakula cha mchana kilichoandaliwa kwa ajili ya wachangiaji wote, Lulu alionekana akirudia kuchukua msosi kwa zaidi ya mara tatu (alikula sahani tatu).
TURUDI MSIBANI
Baadhi ya watu waliokuwa msibani hapo walimshangaa Lulu kwa kuporomosha matusi hayo ya nguoni wakati akijua kuwa yeye ni kioo cha jamii na baadhi ya maneno machafu aliyoyatamka hadharani hayaandikiki gazetini.

MSIKILIZE LULU
“Siwapendi nyinyi waandishi hasa wewe (akamtaja jina). ‘I don’t want your f**** story dude, go to hell with you’re f**** shit,” alisikika Lulu akitamka matusi hayo. (hatuwezi kuyatafsiri kwa sababu za kimaadili).

WAOMBOLEZAJI SASA
Mamia ya waombolezaji waliokuwepo eneo la msiba huo walionesha kushangazwa na kitendo cha binti huyo aliyejipatia umaarufu kutokana na kuigiza kwake.

Baadhi yao walidai hali hiyo haikuwa ya kawaida na huenda alikuwa ‘amepata kiburudisho’ (alikunywa pombe).
“Sasa binti si uende ndani ukakae? Hapa ni msibani halafu wewe unasema maneno kama hayo, huoni kama unasumbua akili za wenzako?” mzee mmoja alisikika akisema wakati Lulu anaondoka.

“Unajua hawa mastaa wa Bongo mimi nimeshawajua kwani nawafuatilia sana, wakiandikwa kwa mazuri meno thelathini na mbili nje, wakiandikwa kwa mabaya timbwili kama hili.
“Hiyo habari anayoilalamikia mimi niliiona kwenye gazeti tena ilikuwa na picha sasa alichokereka ni nini, si kweli au?” alisikika mwombolezaji mwingine.
Mwombolezaji mwingine alisema Lulu anaweza kuwa na hoja lakini inakufa kwa vile kama habari ilimkera alipaswa kumtafuta paparazi huyo kwa wakati wake au afike Ofisi za Global badala ya kujianika hadharani huku akidai siku hizi amebadilika.
KWA NINI ALIKEREKA?
Habari zilizopatikana baadaye zilisema kuwa, Lulu alihamaki kumwona mwandishi huyo aliyeandika habari zake hizo za kula sahani tatu, kwani tangu kutoka kwa stori hiyo amekuwa akitaniwa na mastaa wenzake wakimwambia ‘yeye ni mbaya sana kwenye mechi za ugenini’.
Tafsiri hiyo ni kwamba, Lulu amekuwa akila kupitia kiasi kwenye ‘minuso’ (minuso ni vyakula vya bure kwenye shughuli).

AJITENGA NA BONGO MOVIE
Wakati huohuo, Imelda Mtema anaripoti kuwa, baada ya kufika ndani ya nyumba ya akina Wema, Lulu alionekana kutotaka kujihusisha na baadhi ya wasanii wenzake wa Klabu ya Bongo Movie Unity ambapo alijitenga.

Lulu alijitenga kwa kukaa na mama yake mzazi, Lucresia Karugila na mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa.
Wasanii wa Bongo Movie waliokuwepo ambao hawakupata nafasi ya kupiga stori na Lulu kama zamani ni Jacqueline Wolper, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’, Jennifer Kyaka ‘Odama’,  Rachel Haule, Kajala Masanja na Eshe Buheti.   

Baadhi ya waombolezaji waliokuwemo walinong’ona kuhusu kitendo cha staa huyo kujitenga wakidai kweli sasa amekua.
 “Mh! Lulu sasa amekua jamani, naona hataki kabisa ushoga na watu, alipofika akasalimia na kwenda kukaa na wazazi wake, ni maajabu,” alisikika akisema mmoja wa waombolezaji ambaye jina lake halikufahamika.

Mwombolezaji mwingine alisikika akisema kuwa mabadiliko yote yanayoonekana kwa Lulu kwa sasa ni kazi ya mama Kanumba.
TUJIKUMBUSHE
Mzee Isaac Sepetu alifariki dunia Oktoba 28, 2013 katika Hospitali ya TMJ, Dar alikokuwa amelazwa kwa matatizo ya kisukari.

MAZISHI YA MZEE SEPETU
Mwili wa marehemu ulitarajiwa kuzikwa jana saa kumi jioni Mjini Zanzibar baada ya kusafirishwa kutoka jijini Dar es Salaam alikofia.
Mungu ailaze pema peponi roho ya marehemu. Amina.

LULU APONZWA NA PICHA YA JOKATE

ELIZABETH Michael ‘Lulu’ amejikuta akiambulia maneno makali kutoka kwa mashabiki baada ya kuposti picha ya Jokate na kumsifia katika mtandao wa Instagram.

ELIZABETH Michael ‘Lulu’.
Lulu aliiposti picha hiyo kwa nia njema kabisa ambapo kuonesha kuwa anamkubali Kidoti, alimwagia sifa kuwa ana uzuri wa ziada ndipo wafuasi wa mtandao huo walipotema mbovumbovu.
“Anampiga vijembe Wema huyu, mtoto mswazi sana huyu…mnafiki huyu mimi nishamjua hanipi shida siku hizi,” walichangia wadau tofauti mtandaoni.

HAPPY BIRTHDAY DR.CHENI, HIKI NDICHO ALICHOKIANDIKA LULU

Mwigizaji maarufu Swahiliwood Muhsin Awadhi(Dr. Cheni leo anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa(birthday). Kama kawaida kwa siku muhimu kama hii kwa kila mtu, watu mbalimbali humtakia mhusika afya njema na maisha marefu, mafanikio na kila la kheri huku wengine pia wakitoa au kuelezea hisia zao kwa mlengwa. Elizabeth Michael(Lulu) nae ameamua kumtakia Dr. Cheni kheri ya siku ya kuzaliwa kwa kumuelezea kuwa Dr. Cheni ni mtu muhimu sana katika maisha yake kwakuwa na upendo wa dhati kwake na kumthamini. "Daah..don't even know where to start!!!!okay....umekuwa ni mtu muhimu sana katika maisha yangu...mtu mwenye kunipenda kwa dhati na kunithamani...kila ninapokuwa najaribu kukuelezea huwa nakosa cha kuongea na najisikia kulia tu....!!!nina uhakika sina cha kukulipa zaidi ya kukuombea uishi maisha marefu yenye amani,afya na faraja!!!HAPPY BIRTHDAY DADDY CHENI......♥" alisema Lulu mmoja wa actresses maarufu katika Swahili movies.


Dr. Cheni ndiye aliyemuingiza Lulu katika sanaa kwa kumpeleka Kaole na hata baada ya kukumbwa na matatizo bado yupo bega kwa bega na Lulu. Dr. Cheni ni mmoja wa waigizaji wenye mchango mkubwa katika tasnia ya maigizo na filamu nchini akiwa ametamba na michezo kadhaa kipindi hicho ITV na baadaye katika filamu na kupelekea waigizaji wengi chipukizi kuhamasika kuingia katika sanaa ya filamu. Baadhi ya filamu alizoigiza ni pamoja na Nipende Monalisa, Danger Zone, Majanga, Jessica na nyinginezo. 


HAPPY BIRTHDAY Muhsin Awadhi(Dr.Cheni)
 

                                       Lulu na Dr. Cheni

LULU AONEKANA KUUHESHIMU MWEZI MTUKUFU

 
LULU AKIWA KATIKA MUONEKANO TOFAUTI NA TULIVYOMZOEYA KATIKA MWEZI HUU MTUKUFU AMBAPO WAISLAMU WAPO KATIKA MFUNGO:

BAADA YA LULU KUA KIMYA KWENYE SOKOLA FILAMU


Baada ya kujinyakulia tuzo ya msanii bora wa kike kutoka Zanzibar International Film Festival 2013 (ZIFF) kupitia filamu ya woman of principle, Elizabeth Michael aka Lulu anatarajia kuja na filamu yake mpya itakayoitwa “foolish age”.
Kupitia filamu ya woman of principle, Lulu alijiongezea umaarufu na kuonyesha uwezo mkubwa wa kushirikiana na mastaa wa kubwa kama Ray na Nargis. Foolish age itajaa mastaa mbalimbali wenye uwezo mkubwa wa bongo movie.
Lulu bado ajafunguka sana kuhusiana na location ya foolish age wala tarehe itakayo dondoka sokoni.

 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger