Akizungumza katika kituo kimoja cha runinga cha jijini Dar hivi karibuni, Ray alisema licha ya kuwa Lulu alikuwa anastahili kuigiza katika sinema ya Woman Principle miaka kadhaa iliyopita, aliona Lulu anafaa kutokana na umakini wake lakini akaona bora amchukue Miss Tanzania namba 3, 2003, Nargis Mohammed kwa kuhofia kupata aibu ya kuoneshana malavidavi na Lulu.
Vincent Kigosi ‘Ray’.
“Lulu alikuwa na uwezo wa kumudu kipengele hicho, kipindi hicho
alikuwa mdogo sana, niliona ni jambo la aibu kidogo kumbusu mdomoni
mtoto mdogo kama yeye halafu ni kitu ambacho jamii itakaa ikitazame
nikaona bora nimchukue Nagris, Lulu nikampa sini nyingine,” alisema Ray.Aliongeza kuwa, kikubwa kilichomfanya avutiwe kucheza na Nagris ni kwa sababu ni mwanamke ambaye katulia na hana skendo hivyo itamuongezea heshima na mvuto wa kazi yake katika jamii.