Mtuhumiwa wa Uwizi aliejitambulisha kwa jina la Juma Hamis huku
akiwa na Kitambulisho cha Kazi cha Idara ya Usalama wa Taifa chenye
jina la Kenedy Magige,akiwa amewekwa chini ya Ulinzi mara baada ya
kunaswa Usiku huu kwenye Hoteli ya Picolo,Kawe jijini Dar es Salaam,
Kitambulisho alichonashwa nacho Mtuhumiwa huyo kinaosomeka namna hii.
Kava ya nje ya Kitambulisho hicho kinaonekana namna hii.
Watuhumiwa hao wakiwa chini ya Ulinzi wa Polisi.
Kitambulisho hicho kinavyoonekana kwa nyuma.
Mtuhumiwa wa Uwizi
aliejitambulisha kwa jina la Juma Hamis huku akiwa na Kitambulisho cha
Kazi cha Idara ya Usalama wa Taifa chenye jina la Kenedy Magige.
Mtuhumiwa mwenza wa Tukio
hilo la Wizi,aliejitambulisha kwa jina la Takula Manyenga mwenye umri wa
Miaka 28,akidhibitiwa kwa kufungwa kamba mara baada ya kukamatwa Usiku
huu kwenye Hoteli ya Picolo,Kawe jijini Dar es Salaam.
Watuhumiwa wote wawili wakipakiwa ndani ya Gari la Polisi kutoka katika Kituo cha Kawe,Jijini Dar es Salaam.
Watuhumiwa hao wakiwa ndani ya gari la Polisi.
Askari Polisi wakiwa eneo la tukuo kuhakikisha Usalama unapatikana eneo hilo.
Mara wakashushwa kwa muda na kuelekea kwenye Gari lao walilokuja nalo watuhumiwa hao.
Askari Polisi wakiwa na
Watuhumiwa hao wakati wakiendelea na Ukaguzi ndani ya Gari hilo aina ya
Toyota Prado lenye nambari za Usajili T 445 BCY.
Askari Polisi wakiendelea
na Ukaguzi ndani ya Gari hilo,ambapo ndani ya Gari hilo kulikutwa na
Simu zaidi ya kumi ambazo zilichukuliwa na Polisi hao.
Gari walilokuwa wakilitumia Watuhumiwa hao.
Wakipelekwa kwenye Gari la Polisi tayari kwa safari ya kwenda Kituoni.
Ulinzi mkali kwa watuhumiwa hao.
Msafara wa kuelekea kituoni.
Watu wawili wanaotuhumiwa
kuwa ni wezi a.k.a Wapigaji/Matapeli wamekamatwa Usiku huu kwenye hoteli
ya Picolo,Kawe jijini Dar es Salaam.
Watu hao ambao wamekamatwa
ni Bw. Takula Mayenga mkazi wa Mbezi Temboni na Bw. Juma Hamis ambaye ni
mkazi wa Tabata wakiwa na nyaraka tofauti ikiwemo kitambulisho cha
Idara ya Usalama wa Taifa, kadi za benki pamoja na simu zaidi ya
kumi,wakiwa katika harakati za kumtapeli mwanadada mmoja
aliejitambulisha kwa jina la Rebecca ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo cha
Biashara cha CBE,Mkazi wa Mbezi Beach jijini Dar es Salaa .
Akisimulia tukio dada huyo
ambaye alipatwa na tukio hilo la kutapeliwa Ijumaa ya wiki iliyopita
alisema kuwa, ilikuwa ni Ijumaa iliyopita wakiwa wamekaa katika fukwe
wakipunga upepo ndipo alipokuja tapeli huyo na kukaa nao na baadae
walimwekea madawa ya kulevya na kuondoka na dada huyo kwenda kumtupa
baharini