Akipiga stori na mwandishi wetu hivi karibuni, Aunt alisema mumewe, Sunday Demonte alikamatwa kutokana na viza yake kuisha ambapo alishikiliwa kwa muda na alipokamilisha taratibu za ‘kurinyuu’, aliachiwa.
“Nashangaa sana mambo haya yamevuma kuwa mimi nimemuacha mume wangu amefungwa, ukweli ni kwamba mume wangu yuko huru na hata sasa ukitaka ongea naye, ni mwanamke gani atakuwa na furaha hivi wakati mumewe ana matatizo?” alihoji Aunt.
Aunt akiwa na mumewe.
Katika mistari mingine, Aunt alisema watu wengi wanatamani kuona
ameachika au kujua mwenendo wa maisha yake na mumewe lakini
wanajidanganya kwani yeye ni mwanamke aliyeamua kuolewa na amefundwa
hivyo wataambulia patupu.“Siyo rahisi mimi kutoa siri ya maisha ninayoishi na mume wangu, ni makubaliano yetu. Kimsingi ndoa yetu iko imara, watasubiri sana na watachoka wenyewe,” alisema Aunt