Akipiga stori na Centre Spread mama Kanumba alisema hayo kutokana na mastaa wengi kutamani awape nafasi ya kucheza kama Kanumba katika filamu yake anayoiandaa inayohusu maisha ya mwanaye tangu utotoni, na kudai katika wote hajaona mwenye kigezo cha kumpa nafasi hiyo.
Marehemu Steven Kanumba.
“Siyo kwamba hawana kiwango kizuri cha kumfikia mwanangu, isipokuwa
kwa mtazamo wangu naona nikimshirikisha staa yoyote katika kipengele
hicho nitakuwa nimevurunda kazi yangu…nitaandaa tamasha maalumu la
kumsaka kijana anayefanana na Kanumba,” alisema mama huyo.