Jeneza la marehemu Kihiyo likipelekwa kaburini tayari kwa mazishi yake yaliyofanyika leo jioni makaburi ya Mwinyimkuu Magomeni.
Jeneza la marehemu Kihiyo likipelekwa kaburini tayari kwa mazishi yake yaliyofanyika leo jioni makaburi ya Mwinyimkuu Magomeni.
Jeneza
la marehemu Kihiyo likiwasili eneo la makaburini tayari kwa mazishi
yake yaliyofanyika leo jioni makaburi ya Mwinyimkuu Magomeni.
Kaburi la marehemu Kihiyo linavyoonekana kwa ndani.
Mwili wa marehemu Kihiyo ukiwa ndani ya kaburi.
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
UBAGUZI
wa wasanii Tanzania umedhihirika leo baada ya kususia msiba wa msanii
mwenzao Hassan Kihiyo aliyezikwa saa kumi za jioni katika makaburi ya
Mwinyimkuu, Magomeni.
Msiba
huo ulihudhuriwa na wasanii wachache, hasa wale wasiokuwa na majina
makubwa, licha ya Kihiyo kujitoa mara kwa mara katika matatizo ya
wasanii wengine Tanzania.
Kihiyo
alifariki jana jioni katika Hospitali ya Wilaya Temeke alipokuwa
amelazwa akipata matibabu na kupeleka huzuni kubwa kwa baadhi ya wasanii
na mashabiki wanaomuunga mkono.
Mazishi
ya msanii huyu hayakuwa na tofauti na watu wengi, licha ya kucheza
filamu kadhaa na kushiriki kutengeneza movie za wasanii wengine kwa
namna moja ama nyingine. Kihiyo alicheza filamu zaidi ya nne, ikiwamo
ile Mother House, Kaburi Moja, Chanzo ni Mama, Where is God, My Book na
nyinginezo.
Wadau
na wasanii wachache waliohudhuria msiba huo ni pamoja na Emmanuel
Shija, John Mtitu, John Lister, mtunzi wa filamu na maigizo Tanzania,
Muddy Kimindu Kulinyangwa ambaye pia ametunga nyimbo mbalimbali za
taarabu kama vile Domo la Udaku la T-Moto Taarab, Nani Kama Mama wa Isha
Mashauzi na nyinginezo.
Mbali
na kususia kwa wakali wa filamu Tanzania, mazishi ya Kihiyo yalifanyika
vizuri na kutanguliwa na swala, ambapo msikiti haukuwa mbali na
nyumbani ulipokuwapo msiba pamoja na sehemu ya makaburi aliyozikiwa
marehemu.
Wasanii
wa Tanzania kwa mtindo huo wameonekana kubaguana wenyewe kwa wenyewe,
wakiangaliana usoni na wale wenye majina makubwa zaidi ndio wanaoishi
kwa kujuliana hali, hasa katika matukio ya misiba wakiamini vyombo vya
habari, wadau na mashabiki wataendelea kujazana kwa ajili ya kutaka
kuuza sura.