Mbunifu
wa mavazi nchini, Martin Kadinda amesema kuwa amekuwa akikutana na
changamoto kutoka kwa wanaume wengi wanaodhani kuwa yeye ni shoga na
kufikia hatua ya kumtumia ujumbe wa kumtaka kimapenzi.
“Kila
mtu anakuwa na maswali yake anaya-raise kutokana na anacho kifikiria
katika akili yake, Watanzania tunatabia ya ku-create situation katika
akili zetu halafu we want everybody to accept.Kwamba mtu tu anaamka
asubuhi may be ana matamanio na wewe anaanza ku-raise hilo swali aone
jibu litakuwa ni nini. Wapo wengi (wananitamani) wako hivyo, facebook,
Instagram mtu atakutumia namba yake, hakwambii lakini unaona kabisa
huyu, nakukubali sana I wish siku moja uje nyumbani kwangu au can I come
to your place, mimi sitakagi hata kwenda huko najua nitajiuliza
imekuaje mpaka imefikia hivi, basi nasema sawa. Kwa sababu mimi facebook
nakuwa mkweli sijawahi kujibu mtu tangu 2012, I have a person huwa
anazipitia, akiulizia mtu maswala modelling mpe namba ya fulani, mambo
mengine binafsi usiwajibu achana nao, kwa sababu mara ya kwanza nilikuwa
ninadhani I should meet these people talk to them this is not right but
nikaona unapoanza kuwa unajihusisha ndipo unapojikuta unaanza kuingia
bila kujua” Martin Kadinda aliambia Sporah Show.
Pia Martin amesema kuwa ana mpenzi wake ambaye hapendi kumuweka wazi ili kulinda heshima yake.
“Ukishakuwa
maarufu na mtu wa karibu yako atakuwa maarufu, she’s not already kwa
hiyo kitu yakuingia kwenye hiyo cycle kila siku wanamuona kwenye
magazeti kwenye Instagram haiko hivyo. Ndiyo maana hata nikiweka picha
yake Instagram nitaweka picha yake moja kwa miezi sita, yupo hata
ukitaka kumuona kwenye Instagram yangu yupo, first lady wa martin huyu,
lakini cycle yake na maisha yake siyo mtu wa kukaa kwenye media nadhani
ni kwa sababu ya future ya kazi atayokuja kuifanya kwaiyo anajitaidi
kuwa pembeni… Mara ya kwanza alishawahi kuniuliza alipita kwenye comment
za watu kwenye blog fulani akasoma, akaniambia najua hii ni Watanzania
walivyo, as long nakutambua mwanaume wangu ni mtu wa namna gani I don’t
care about these people” Alimaliza Martin