Imebainika
kwamba waimbaji wa muziki wa Injili nchini, Flora Mbasha na
mumewe, Emmanuel Mbasha hawajapatana kama ilivyodaiwa awali na
taarifa zinasema kuwa mwanadada huyo ameanza maisha yake
kivyake kwa kupanga nyumba nyingine mbali na mumewe….
Habari
za kuaminika toka ndani ya familia ya Flora zinasema kuwa
msanii huyo amekuwa na wakati mgumu wa kumsamehe mumewe
kutokana na tabia zake chafu ambazo zimekuwa zikiutesa moyo
wake na sasa anang’ang’ania kumchukua mwanaye…..
“Hivi
karibuni iliripotiwa kuwa wanandoa hao wamepatana lakini ukweli
ni kwamba hakuna kitu kama hicho,mwanamke amepanga chumba chake
hapa Dar es Salaam na kumwachia kila kitu mumewe ambaye sasa
ana haha kumchukua mwanaye ili aishi naye,” kilisema chanzo cha habari.
Lakini
upande wa pili, mume wa msanii huyo hivi karibuni alieleza
kuwa ugomvi baina yao ulianza kutokana na kuchepuka kwa mkewe,
huku akipeleka shutuma kwa mchungaji wa kanisa la ufufuo na
Uzima, Josephat Gwajima ambaye ni maarufu kwa vitu ambavyo ni
tofauti na huduma zake….
Emmanuel
Mbasha tayari alishatoa waraka wa wazi kwenda kwa mchungaji
huyo, akimtaka kukaa mbali na ndoa yake jambo ambalo bado
halina mrejesho chanya kwani wawili hao Flora na Gwajima
wameendelea kufanya kazi pamoja kitu kinachopelekea Emmanuel
kuona bado kuna kitu kinaendelea kati yao….
Kutokana
na hali hiyo, mume wa Flora amekuwa mgumu kumtoa mtoto wake
akihofia kulelewa na mtu ambaye kwake anamchukulia kama adui
wa familia yake…
“Imekuwa
ngumu sana kwa Emmanuel kumwachia mtoto wake katika hali hii,
hata kama ni wewe unamuachiaje mtoto wako kipenzi aende kwa
mwanamke ambaye ni msaliti,” alisema ndugu wa karibu wa
Emmanuel Mbasha