Mwenyekiti wa bongo movie Unity, Steve Nyerere amechukizwa na watu wanaotumia mitandao vibaya na kwa kumzushia kuwa ni shoga.
Steve Nyerere kupitia akaunti yake ya facebook ameandika:
Napenda kuchukua fursa hii kuongea
machache na kama mtaboa mtu naomba samahani najua binadamu tumezaliwa
tofauti sana kuna wale wanaogopa zambi na kunawale wanopenda zambi mimi
daima nasema izo ni changamoto tuuu ok nimepata taarifa umu umu kwenye
mitandao yetu ya kijamiii hususani huuu kwamba kuna binti anaitwa zainab
ananichafua na kuniandika mambo ambayo ayana tija kwangu.
Nazani ata kwake kwamba mimi shoga
anauhakika hahahahaha nimecheka sana kupata izi taarifa nataka kuwapa
taarifa ndugu zangu kuna msemo unasema mti wenye matunda ndio unaopigwa
mawe na mkanya mara moja aache mara moja kwani naimani anapoteza muda tu
habari hizo si zakweli kabisa ila namtakia laheli kwahili jambo
analonitendea mimi nasema namwachia mola akumbuke nafamily mke na watoto
mama dada zangu kiukweli najisikia vibaya sana mi nasema asante”.
Baada ya kuandika kauli hiyo, Steve Nyerere ameuambia mtandao wa bongo5 kuwa kuna watu wameamua kumchufua baada ya kujionyesha wazi kwenye siasa.
“Watu wananitumia meseji mbaya, eti mimi nimetumwa na viongozi, mara sijui mimi ni shoga, jamani hakuna mambo kama hayo, nawataka watanzania wajue hayo ni mambo za uzushi, sijui ata yametoka wapi” Alisema Steve Nyerere