JESHI la Polisi mkoani Morogoro limemkamata msanii nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kwa kosa la kuendesha gari kwa mwendo wa kasi wakati alipokuwa akiwahi shoo ya Fiesta iliyofanyika mjini hapa Jumapili iliyopita.
Kwa mujibu wa askari mmoja wa kikosi cha usalama wa barabarani aliyeomba hifadhi ya jina lake kwa kuwa si msemaji wa jeshi hilo, walimkamata msanii huyo eneo la Msamvu baada ya kugoma kutii amri ya kusimama kama alivyotakiwa na askari wa barabarani ‘trafiki’ eneo la Nanenane nje kidogo ya mji.
“ Msanii huyo akiwa na gari lake aina ya Alteza alitumia vibaya barabara na kuendesha gari kwa mwendo kasi kiasi cha kupiga ovateki eneo lisiloruhusiwa na askari alipomsimamisha akagoma kutii amri hiyo.
“Askari huyo aliwajulisha wenzake kwa njia ya simu ya upepo na Nay alipofika Msamvu alikamatwa na kupigwa faini papohapo,” alisema askari huyo.
Baada ya kulimwa faini ya shilingi 30,000 msanii huyo aliachiwa na kuwahi shoo ya Fiesta iliyokuwa ikifanyika ndani ya Uwanja wa Jamhuri ambapo wasanii mbalimbali walitoa burudani ya kiwango cha juu