Lissu alisema njama hizi ndio zilizopelekea mpaka mashtaka ya Ugaidi ambapo katika mahojiano yake ya Star Tv akiwa na akina Mwigulu Nchemba Zitto hakukanusha, pia aliandika kwenye mitandao kuwa Chadema imtose Wilfred Lwakatare
Lissu aliongeza kuwa Zitto mpaka sasa ana magari mawili ya Nimrod Mkono
na Mkono mwenyewe ndiye amewaambia taarifa hizo. Mkono amewaambia kuwa
amempa Zitto hela nyingi sana na Zitto alishiriki moja kwa moja kumzuia
mgombea wa Chadema katika Jimbo la Nimrod Mkono .
**
Lissu anasema nimepewa magari 2 na Mzee Mkono. Anasema kaambiwa na Mkono. Naamini Mkono alimwambia pia mwaka 2005 alimpa Freeman Aikaeli Mbowe tshs 40m ili Mbowe asifanye kampeni Musoma vijijini.
Nadhani alimwambia pia mwaka 2008 (baada ya orodha ya mafisadi kutangazwa 2007) Mkono alimpa Freeman tshs 20m za uchaguzi wa Tarime na Freeman akasema kwenye chama ametoa mkopo na akalipwa.
Nadhani alimwambia pia kuwa Mwaka 2010 Mkono alimpa Mbowe tshs 200m za kampeni ya Slaa.
Pia
hakusahau kumwambia kuwa Rostam Aziz alimpa Mbowe tshs 100m za kampeni.
Lissu anajua kuwa gazeti la Tanzania Daima limeanzishwa na fedha za
chama kutoka Conservative party?
Nimefanya internship yangu kwa
Mkono and Company Advocates kuhusu masuala ya mikataba. Mzee Mkono ni
Mzee wangu na alisaini petition ya kumtoa Waziri Mkuu Pinda.
Lissu
awaambie waliyemtuma wamwambie ukweli wote. Lissu ajue yeye ni
kifaranga tu, Mimi namtaka mama wa kifaranga ajitokeze. Aeleze aliingia
deal gani na Kinana na Sumaye mwaka 2005 kufuatia deni lake NSSF. Aweke
wazi mkataba kati yake na NHC kuhusu nyumba ya Umma ilipo Club
Bilicanas.
They must know I am not a push over. Chacha died, I won't.