Search in This Blog

CHOKOCHOKO ZA MADAHA KWA DIAMONDA SASA KWISHA, HII NI BAADA YA KUPATA SHAVU LA MILLION 200


Ile record label maarufu ya muziki afrika mashariki - candy n candy imechapa fimbo nyingine baada ya kufanya deal ya mtonyo mrefuu na kampuni maarufu ya  kusambaza filamu afrika mashariki na kati, (Jina kapuni ) kwa ajili ya kusambaza filamu ya “The gal bladder”  ambayo imechezwa na mwigizaji baby madaha akishirikiana na waigizaji wengine toka kenya.

Kama alivyonukuliwa toka mtandao mmoja maarufu wa habari Afrika Mashariki, msemaji wa kampuni hiyo amesema imekua neema kwao kufanya kazi na kampuni kubwa kama candy n candy films ya nchini kenya, na hiyo itapanua wigo wa ukuaji wa tasnia ya filamu afrika mashariki hususani kenya na tanzania..deal hiyo yenye thamani ya shilingi za kitanzania milioni mia mbili ( mil.200 )inakua moja ya mikataba minono zaidi kufanywa east africa kutoka kwa  kampuni kwenda kwa kampuni kwenye upande wa filamu.
Hiyo inachukukuliwa kuwa moja la pigo la kukata na shoka kwa  kampuni pinzani grandpa records nayo ya nchini kenya ambayo kwa muda mrefu imekuwa ndani ya tasnia ya burudani kwa takribani zaidi ya miaka kumi  bila kuleta mabadiliko yoyote katika tasnia nzima ya burudani,jambo ambalo  candy n candy imeweza kufanya ndani ya miezi mitano tu,katika kutengeneza muziki wa kimataifa bila kusahau project yao ya sasa “highly budget movie   the gal bladder”….ni mfano wa kuigwa kutoka kwa candy n candy records label kuzalisha kampuni tanzu ndani yake ya candy n candy films ambayo itakuwa ikidili na filamu.
Mbali na hayo kampuni hii ina plans za kuanzisha kipindi matata cha runinga ambacho kitakua kikirushwa  Afrika Mashariki yote ,ambapo kama kawaida huwa hawachezi mbali host wake atakua first lady wa candy n candy mwanamuziki,mwigizaji,mwanamitindo na mtangazaji baby madaha”the queen of swaggz”,ikumbukwe hivi karibuni alilamba mamilioni ya shilingi kupitia mkataba wake na kampuni hiyo.
kaaazi kweli kweli…….yetu macho wabongo mpoooo????
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger