Kuna baadhi ya wanaume hawajui
jinsi ya kuzungumza na mwanamke au msichana. Kwa njia hii wanaume wengi
wanaishi maisha ya bila kumvutia mwanamke yeyote.
Hapa kunanjia 10 utakazozitumia wewe mwanaume ili kuhakikisha humkwazi mwanamke unayempenda mnapokuwa katika mazungumzo ;
1. Wakati ukizungumza nae,
jaribu kuzungumzia "hisia" kama vile kumbu kumbu yako ya utotoni,
matarajio ya baadae au matamanio yake. Mada hii ya mazungumzo yenu
yatafungua milango ya hisia zake ghafla.
2. Wanawake huhitaji
mwanaume asiyekuwa na uoga wa kuwamiriki na kuwaongoza. Wakati
unazungumza na mwanamke tawala mazungumzo yenu na kamwe usimpe nafasi ya
yeye kuanza kufikiri kuwa nini ulichokuwa ukizungumzia.
3. Kuwa makini wakati
unapokuwa ukizungumza nae huku akikupatia majibu yasiyo na hisia zozote
za mapenzi. Hapo utajua kunakitu, hivyo kama kwa bahati mbaya uko nae
karibu kiasi cha kugusana, basi jisogeze pembeni wakati ukiwa unaendelea
kuongea ili asishtukie au unaweza kumuona hayuko sawa katika utoaji
majibu.. kwa kawaida atakuonyesha ishara, hivyo kuwa nazo makini.
4. Kumbuka hii kauli mbiu
"Ucheshi/vituko si mapenzi". Wanawake huvutiwa sana na wanaume wanaoweza
kuwafanya wawe na furaha muda wote. Usijikite zaidi katika kufanya
utani unaopita kiasi na kusahau ulichokuwa unaongea. Bali jikite zaidi
katika mambo yanayomfanya ajisikie kuwa na msisimko na starehe wakati
ukonae.
5. Zama katika undani wa
mazungumzo baina yako na yeye. Mwanamke huendana na mwanaume asiyekuwa
muoga wa kuzungumzia mambo binafsi kwa ukaribu.
6. Wanawake wengi hupenda
kujua maoni yako kuhusiana na jinsi unavyomuona. Mwambie vitu
unavyoviona kutoka kwake, lakini jaribu kuwa makini ili usitamke vitu
vingine vitakavyo msababishia apoteze furaha.
7. Epuka kumpa ofa nyingi
mwanamke, mwanamke huwa na mashaka na mwanaume anayempatia vitu vingi
kwa wakati mmoja ama kila mara. Kwasababu atafikiri vitu unavyompatia ni
kutaka kumvutia tu ili umpate kiurahisi. Kitu ambacho baadae kitaleta
madhara makubwa.
8. Kama unahitaji kujua
njia nzuri ya kuweza kuongea na mwanamke au msichana bila kumfanya
asikudharau au kuboreka, basi usitumie njia ya kumuuliza maswali mengi
katika mazungumzo yenu. Bali jaribu kueleza mawazo yako kuhusu vitu
flani.
9. Kumbuka kauli juu ya
kuuliza maswali: Badala ya kumuuliza "wewe umekulia wapi?", uliza
"unaonekana kama hujakulia maeneo haya!" Hii itakusaidia wewe kufanya
uchunguzi juu yake bila yeye kujua.
10. Usifiche utambulisho
wako - zungumza vitu kutoka katika hisia zako, onyesha uhalisia wako
katika kuzungumza na usitumie mikogo ya mtu yeyote.
Njia bora ya kufikiria jinsi ya kuzungumza na mwanamke, ni kutambua njia
sahihi ya mazungumzo ya furaha na yakimahaba utakayopenda kuitumia,
isipokuwa usimuige mtu. Kuzungumza na mwanamke sii vigumu bali nikujua
ni vitu gani hasa mwanamke hapendi kuvizungumzia na vitu gani anapenda
kuvisikia. Fuata maelekezo hapo juu utaona matunda yake...kisha rudi toa
maoni yako hapa.
MUHIMU: Maelekezo haya yote yatafanikiwa kwa mwanamke mwenye
kuhitaji mapenzi ya kweli - yani sio kwa wanawake wanaolenga kuchota
pesa kwako na kutokomea. Hivyo kuwa makini sana.