BAADA YA KUZUSHIWA KIFO, HIKI NDICHO ALICHOSEMA MSANII SAIDA KAROLI.
Baada ya taarifa kuzushwa
kuwa Mwanamuziki wa asili, Saida Karoli amefariki katika ajali ya meli habari za uhakika ni
kuwa Saida Karoli wala hayuko mahala popote jirani na Ziwa
Victoria.
Baada ya kuweko Dar es Salaam wiki iliyopita, Saida na
kundi lake walikodishwa na kuelekea Makongorosi Chunya mahala aliko
mpaka asubuhi hii.
Saida Karoli anasema "sina mpango wowote wa kufa hivi karibuni".