The Tianhe-2, ambayo maana yake ni Milky Way 2, iliundwa na chuo kikuu cha technolojia ya ulinzi cha nchini humo katika jiji la Changsha.
Taarifa hiyo ilichapishwa kwenye ripoti ya TOP500 – ripoti ya kila mwaka inayoorodhesha supercomputer zenye kasi zaidi duniani.
Kwa mujibu wa orodha hiyo, Marekani imechukua nafasi ya pili, tatu, tano, sita na ya nane.
K computer ya Japan imekamata nafasi ya nne huku Juqueen na SuperMuc za Ujerumani zikikamata nafasi ya saba na ya tisa.