Search in This Blog

K-LYINN AACHA MZIKI, SIKIA SABABU ZAKE

Ulishawahi kujiuliza kwanini Miss Tanzania wa zamani, mrembo Jacqueline Ntuyabaliwe ‏aka K-Lyinn aliacha muziki? I mean seriously, why? af54d9c4c20c11e2950322000a1fcea7_7
Pamoja na kufanikiwa kutoa hits kama Nikipata Wangu, Crazy Over You na hata Nalia kwa Furaha ambayo ni miongoni mwa video za kitanzania zilizoangaliwa zaidi kwenye Youtube ikiwa na hits 1,147,795+, mrembo huyo aliamua kukaa kimya kabisa. Ama ni kwasababu tayari ‘ameshapata wake’ aliyefanikiwa kuleta naye duniani watoto mapacha? Hell NO!!
4a46bf00bb0611e2b9a022000a1fa535_7
Baada ya kuulizwa sana swali la kwanini aliacha muziki, hatimaye leo K-Lyinn ambaye ni mkurugenzi mtendaj, MD wa kampuni ya interior design ya Amorette Ltd, ameamua kuisema sababu.
“Huwa naulizwa sababu ya kuacha muziki,mojawapo ilikua ni ukandamizwaji na kutopewa haki kama msanii.Natumaini waliobaki watapigania haki,” ametweet K-Lyinn.
Swali ni JE! Haki anayoisema ikipatikana atarejea tena kwenye game? Hatupati picha tukisikia single yake mpya baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu. We miss you K-Lyinn.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger