Nilimpokea vizuri nikamfundisha kazi za nyumbani, na kumuelekeza matumizi ya vitu mbali mbali vya nyumbani kwani hakujua hata jiko la gas linawashwa vipi..Nilimfundisha mapishi mbali mbali ambayo alikuwa hajui kupika..
Alikuja akiwa na begi dogo la marlboro lililokuwa na nguo chache za kuvaa, nilimpa nguo zangu nyingi ambazo zilinibana kwani baada ya mimi kujifungua mwili wangu uliongezeka mara dufu...nikamfundisha usafi wa kuoga asubuhi na jioni ili awe smart na aweze kukaa na watoto akiwa msafi...
alikuwa msikivu na hakuwa mjeuri, niliishi naye kama ndugu yangu na hakika ungenikuta nae tunavyopiga stori usingedhani km ni house girl...kuna watu walijua yule ni ndugu yang kwa jinsi tulivyokuwa tunapatana....nikiwaambia ni house girl hawaamini..
Tuliishi kwa vizuri na hatukuwahi kugombana hata siku moja kwani kwa kiasi kikubwa alitimiza majukumu yake niliyompangia...
Baada ya muda nikaona nimsaidie zaidi kwani pamoja na kuwa ni house girl wang lkn pia alikuwa yatima kwani wazazi wake wote walishafariki dunia..Na pia mtt wangu wa mwisho kwa wakati huo alianza shule kwa hivyo angepata fursa ya kujiendeleza kwani hakukuwa na mtt mdogo aliyebaki nyumbani..
Nikamtafutia shule ya QT ili asome masomo ya sekondari ambayo nilimgharamikia kila kitu..akaanza kusoma hiyo shule kwa makubaliano kwamba atafanya kazi zake zote asubuhi na mchana aende shule..
Nilipokuwa nasafiri na watoto wakati wa likizo au kwenda mapumziko mikoa mbali mbali au nje ya nchi naye pia nilimchukua tukawa pamoja naye..(kumbuka kuwa hapo nyumbani kwangu nilikuwa naishi na watu wengine ambao ni ndugu zangu lkn niliwaacha wao nikawa namchukua yy)
Kila nilipokuwa nasafiri kikazi nilikuwa nawaletea watoto wangu zawadi na yeye pia namletea..
Wakati wa sikukuu nilikuwa nawanunulia watoto wangu nguo mpya na yeye pia namnunulia..na ili kumfanya ainjoi sikukuu yake zaidi nilikuwa nampa pesa ambayo simkati kwenye mshahara wake..
Kila j2 alikuwa free kuanzia saa 4 asb hadi saa 12 jioni, nilimruhusu aende popote lkn ikifika saa 12 awe kesharudi..
Kila mwisho wa mwaka nilimpatia nauli na zawadi za kuwapelekea ndugu zake na wadogo zake na alienda likizo
Nilimkatia bima ya afya na yeye akawa anatibiwa aga khan hospital kama watoto wangu
Nilimnunulia simu ya mkononi na kila simu yake ilipoharibika nilimnunulia nyingine
Kabla sijanunua machine ya kufulia aliniambia yeye hawezi kufua nguo na mikono kwani mikono yake inaharibika na kupata fangas nikamtafuta mtu wa kufua nguo ambaye nilikuwa namlipa..
Kila alipofanya kazi ya ziada kwa mfano kuhudumia wageni au siku za sikukuu ambapo kazi ni nyingi nilikuwa namlipa pesa muda huo huo baada ya kumaliza hizo kazi, na mshahara wake mwisho wa mwezi uko pale pale..
Siku moja moja za wk end nilikuwa namsuka kwani kwa bahati nzuri mie najua kusuka mitindo mingi tu...
siku kama sijamsuka basi nampa hela ya saluni/msusi
siku nikienda naye sokoni/supermaket basi hanunui chochote kwa pesa yake, akitaka kitu namnunulia
kila mwaka unapoisha na mwaka mpya kuingia nilikuwa namuongeza mshahara ili naye ajisikie mwenye thamani.
Kwa muda niliokaa naye aliweza kusave na kununua plot baada ya mimi kumshawishi afanye hivyo ili iweze kumsaidia baadae, japo mimi nilimuongezea pesa kdg iliyopelea.
Nilimuahidi kumsomesha hadi chuo kama yeye angependa na kujitahidi katika masomo ili naye awe na maisha yake baadae..
kichwani mwangu nilipanga kumfundisha gari kwani nilishamchukulia km ndugu yangu...hili nilikuwa sijamwambia, nilitaka amalize kwanza elimu ya sekondari.
NOTE
kwa nature ya kazi yangu huwa nasafiri mara kwa mara lkn nikiwa nyumbani lkn huwa sina tabia ya kujibweteka na kumuachia house girl afanye kila kitu...
Kila siku jioni napika chakula cha usiku baada ya kurudi kazini, nikichelewa namwambia apike cha watt na watu wengine, changu na cha baba napika mwenyewe nikifika...mara nyingi mimi na mr tunakula ugali wao wanapenda wali, n.k
nafanya usafi wa chumba changu choote hadi washroom mara 3 au 4 kwa wiki
nafua nguo zangu na za mume wng zote siku ya jumamosi.
siku ya jumamosi na jumapili naingia jikoni kuanzia asb hadi jioni, except kama nimeenda kazn au nimepata dharura..siku za wk end asb huwa natengeneza mchemsho kwa ajili ya familia....na pia napika mwenyewe chakula cha mchana na usiku..(binafsi huwa sipendi kupikiwa hasa nikiwa nyumbani kwani nahisi km chakula kina kasoro nyingi km atapika m2 mwingine,) kwa ivo huwa naingia jikoni mwenyewe.
ALICHONIFANYIA SASA
Baada ya miaka kadhaa nikahisi kama anabdilika na kuwa jeuri lkn sikujali saana, nilijua tu labda yuko days hivi ambayo wkt mwingine yanasababisha mood kuchange..
Nilikuwa na mpaka leo huwa simruhusu house girl kuingia chumbani kwang kwani usafi na kila kitu huwa nafanya mwenyewe hata kama nina mimba ya kujifungua leo..
Sasa kuna kipindi niliposafiri nilikuta kitanda changu kimetandikwa vizuri mpk nikawa na was was, sbb mume wangu huwa hatandiki wala habadilishi shuka mpaka nirudi safari...Siku moja nilimuuliza mume wng nani kamtandikia kitanda? kwani najua kbs hata km ni yeye katandika hawezi kunyoosha shuka vizuri, mara nyingi mume wng yupo rafu, akaniambia amemuomba house girl amsaidie kutandika, nikamuuliza tangu lini house girl anaingia chumbani kwng? akasema samahani mke wng sitarudia tena...nikanyamaza moyoni nikaanza kuwa na shaka lkn sikufatilia saana... huyo house girl siku zooooote hakuwahi kuingia chumbani na mimi sijawahi mruhusu, iweje kipindi hicho tena nikiwa nimesafiri aingie? hapo alikuwa kashakaa muda wa kutosha na keshakuwa mzoefu ila sio chumbani kwang...ila nikapotezea kwani baada ya hapo ikawa hata nikisafiri nakuta vile vile chumba kipo rafu rafu, hakujatandikwa kama zamani, nikajua ni kweli ilikuwa msaada tu kwa mr na nikafutilia mbali was was wng...
Miezi miwili baadae huyo house girl akaniaga gafla akisema bibi yake ni mgonjwa anaumwa, kwa sbb nilikuwa na namba za simu za ndugu zake nikawauliza wakasema kweli bibi yake anaumwa, nikamruhusu aende kumsalimia..akaondoka, lkn kilichonishangaza ni pale alipokusanya mabegi ya nguo zake zote, viatu vyake vyote n.k nikamuuliza mbona umekusanya kila kitu hutegemei kurudi? akasema anaenda kuwagawia ndugu zake yeye ataanza upya akirudi..na vile alikuwa bado anasoma sikumtilia shaka nikajua atarudi tu...
alipofika kwao tu akanitumia ujumbe mfupi wa simu akisema yeye hatarudi tena na ameamua kusomea huko huko kwao.....aaaaaaaaaahhhhhhhhhhh nilikuwa so much dissapointed sbb wakati huo mi nilikuwa mjamzito tena nakaribia kujifungua...kuna ndugu yng alinionea huruma akaniletea msichana wake anisaidie...
Baada ya muda nikasikia yule house girl wang aliyeondoka ni mjamzito, sikufatilia ila nikajua ndio sbb iliyomfanya aondoke nyumbani kwng..
Baadae akajifungua nikaambiwa, nami nikampigia simu kumpongeza, na pia nikamnunulia zawadi za mtt nikampa mtu ampelekee...lkn pia mara kwa mara nilikuwa nampigia cm na kumsalimia yy na mwanae..
MIAKA KADHAA BAADAE ndio nikaja kujua kuwa huyo mtt wa house girl wangu ni wa mume wangu...
Nilipomuuliza mume wng alikubali na kuniomba msamaha saaaana, akasema huyo house girl kila nilipokuwa nasafiri alikuwa akivaa kanga moja na kujilengesha sana mpk akaingia kwny mtego.
SIWEZI SEMA, MAUMIVU niliyopata hayaelezeki.....
NI MIAKA KADHAA imepita toka tukio hili kutokea, lkn mpaka sasa bado nasikia maumivu yake moyoni....in fact ht jana uck nilikosa usingizi baada ya kukumbuka tukio hili, nikajikuta machozi yananitoka bila kuyazuia...
kwa wema wooooote niliomfanyia huyu house girl kweli hii ndio shukurani yake?,yaaani sina hamu..na mpk leo hii sina hamu...nilibaki nimeshikwa na butwaa..
japo hiyo haijanifanya niwachukie mahouse girl wengine lkn sina hamu nao kabisa hawa watu.