Katika hali ya kustaajabisha mwanaume mmoja mwenye miaka 24 ametolewa
penseli ya kuandikia/kuchorea iliyokuwa ndani ya fuvu la kichwa chake
kwa miaka 15 bila kugundua. Hebu vuta taswira, ile penseli inayotumiwa
na watoto wadogo mashuleni, imekaa ndani ya kichwa cha mtu kwa miaka 15!
Ni jambo la kushangaza right? Inaaminika kuwa mwanaume huyo aliwahi
kupata ajali udogoni iliyopelekea penseli hiyo kuingia kichwani kwake na
kukuwa nayo mpaka alipokuja kufanyiwa uchunguzi na madaktari miaka 15
baadaye.
Baada ya kusumbuliwa na maumivu ya kichwa, baridi, na kutokuona
vizuri kwa jicho moja mwanaume huyo raia wa Afghanistan ambaye hajatajwa
jina, aliamua kwenda hospitali kuchunguza afya yake na penseli hiyo
ilionekana katika scan aliyofanyiwa 2011.
Baada ya hospitali ya’ The Aachen University Hospital’ ya Ujerumani
kumfanyia uchunguzi, ilitoa ripoti kuwa wamekuta peseli ya cm 10 katika
fuvu la kichwa chake ambayo pia ilikuwa imeliumiza jicho lake la kulia.
Baada ya kugundulika kwa tatizo hilo madaktari hao walifanikiwa
kuiondoa penseli katika kichwa chake, na kumpa matibabu ya matatizo
aliyokutwa nayo na ripoti inasema hakukua na madhara makubwa baada ya
matibabu hayo.
Msemaji wa hospitali hiyo Mathias Brandstaedter amesema taarifa
kuhusiana na tatizo la mwanaume huyo imetoka hadharani hivi karibuni
baada ya kuwasilishwa katika mkutano wa madaktari.