Tulienda hivyo, wakati pekee wa yeye kumuona mtoto ni likizo za mwezi mmoja mmoja hadi miwili kati na mwisho wa mihula ya shule hadi alipomaliza form six (gharama zoote za masomo zilikuwa juu yangu), and nikawa nikiishi naye wakati akisubiri majibu ya mtihani. Kwenye mahusiano huwa hakukosi migongano ya hapa na pale na kwa kweli tulikuwa tukishindana katika masuala mbalimbali now and then, but tukawa tukisulihisha na maisha yanasonga. Bahati nzuri akachaguliwa kujiunga na chuo kikuu so still nikabaki na mtoto akaenda chuoni (still nikawa nagharamia masomo yake kwa kila kitu, na bahati nzuri akapata mkopo kutoka Loan Board, so ikawa ahueni kwangu kwani nikawa najazia tu ile percentage ndogo inayobaki). Hapo sasa ndo mabalaa yakaanza kuibuka. Alipofika mwaka wa pili (ambao ndo yuko sasa hivi) kiburi na dharau vikazidi sana nikajua hapa lazima kuna jambo na si dogo. baada ya kumdadisi sana akakiri yeye ana mahusiano na mwanaume mwingine, and since maisha yangu na yeye yametawaliwa na kutoelewana kwingi, ameamua kusonga mbele na kamwe hatarudiana na mimi kamwe.
Na kweli ameshikilia msimamo wako barabara kwani nimejaribu sana kuomba arudi nyumbani tulee mtoto wetu bila mafanikio. Amedai huyo mpenzi wake mpya yuko mwaka wa m wisho (wa tatu) na eti wanapendana sana. Nimeamua kuangalia mbele na kuanza upya mkakati wa kuanzisha familia, though najua nimetoka naye mbali (5 years) and nilidevote resources zangu nyingi kuhakikisha anasoma vizuri. Any advice kutoka kwenu? niendelee kumng'ang'ania kama hali yenyewe iko hivi? Zipi ni haki zangu kama baba wa mtoto ninayemlea (sababu amejaribu kumention habari za kutaka kumchukua mtoto - ana miaka minne sasa