Search in This Blog

NEY WA MITEGO AFUNGUKA ISHU YA TUZO....."WASANII NJAA TU, SITAKI KUBISHANA NA YOYOTE"

Rapper Ney wa Mitego, kupitia wimbo wa "Nasema nao" alifanikiwa kupata tuzo ya wimbo bora wa hiphop, ambao umesababisha malalamiko kwa baadhi ya wasanii wengine ambao wnaona hakustahili kuchukua tuzo hiyo kwa wimbo huo, huku wengine wakidai Fid q anastahili na wengine kudai Stamina ndio anastahili....leo hii Ney mwenyewe kafunga juu ya swala hilo
"aah wasanii ndio wanaolalamika na wameandika kwenye mitandao, lakini mwisho wa siku lazima tukubali matokeo kwamba mziki unabadilika kila kukicha, mi nawaambia wasanii wenzangu kwamba mkiendelea kung'ang'ania huko mtakufa njaa, halafu mwisho wa siku wataendelea kulia tu kila siku kwamba kuna hili mara lile,mi naimani kwamba mashabiki wangu ndio wamenikabidhi tuzo, media zinazosapoti kazi yangu ndio zimenisaidia mpaka mimi nimezungumza na mshabiki wangu popote walipo mpaka juzi nimepata tuzo ya wimbo bora wa hiphop. mi nastahili kupata tuzo, kwasababu kwanza sijui wao wanafanya hiphop gani, wakae waeleze mziki wao wao ni hiphop kwasababu hii na hii na hii na wangu sio hio hiphop kwasababu hii na hii na hii. bwana hiphop ni ukweli na unabadilika kila siku kila kukicha. Mi nawashauri tu kitu kimoja, sitaki kubishana na msanii yoyote, wana njaa, wakiendelea kung'ang'ania huko watakufa njaa, kwanini watu wamemsapoti Ney, kwanini watu wamemsapoti Kala Jeremiah,angalia mashairi ya Kala yako wazi, lakini we unaweka sijui mafumbo ya dizaini gani nani atakuelewa...........
halafu tuzo sio lazima upate tuzo, sio lazima ulaumu, kuna wasanii wakali hawajawahi kupata tuzo lakini hawajawahi kulalamika, kuna wasanii kama Juma Nature, nani anaweza kusimama stage na Nature? sijawahi kumsikia anaongea.....
category moja tu nimewekwa nimetusua wao wanalia, shauri yenu shauri yenu, jipangeni mwakani, mi staki kubishana nao, am the best, halafu wasipoangalia nawatengenezea kiwanda kwa ajili ya kuwaajiri wanapoendelea kuwana na hali ngumu, natengeneza kiwanda ambacho ntawaajiri wasanii  wanaofeli wote kwasababu hawana shughuli za kufanya." amesea Ney.
Pages (38)1234 »
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger