Penny akiwa hospitali.
Imejulikana kwamba mimba anayotamba staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul
‘Diamond Platnumz’ kuwa amempachika mpenzi wake, Peniel Mungilwa
‘Penny’, inadaiwa kuanza kumtesa mtangazaji huyo wa DTV, Ijumaa Wikienda
linashuka nayo.
Habari zisizokuwa na chenga kutoka kwa chanzo chetu ambacho ni mtu wa
karibu wa mrembo huyo, zilieleza kwamba kufuatia hali hiyo, Penny
alikimbizwa kwenye Hospitali ya Regency, Dar wikiendi iliyopita kisha
akalazwa, akachomwa sindano na kutundikiwa dripu.Hata hivyo, habari tulizozipata wakati tunakwenda mitamboni zilieleza kuwa Penny aliruhusiwa kutoka hospitalini na anaendelea vizuri.