Habari
za uhakika ni kuwa muigizaji wa vichekesho nchini maarufu kwa jina la
Masele cha Pombe ni mzima wa afya na hajafariki kama baadhi ya tetesi
zilivyoanza kuenea kwa kasi. Swahiliworldplanet baada ya kusikia tetesi
kuwa Masele amefariki kwa ajali ya gari jioni hii huko Tanga ilibidi
kutafuta ukweli kuhusu muigizaji huyo maarufu na kufanikiwa kupata
habari za kina kupitia Kabuti Onyango ambaye ni cameraman maarufu wa
filamu za kitanzania. Kabuti ambaye ni mtoto wa Mzee Onyango ambaye ni
muigizaji mkongwe
nchini
amesema kuwa amezungumza na baba yake(Mzee Onyango) muda mfupi uliopita
ambaye yupo Tanga na jibu ni hili " baba yupo Tanga mzee onyango na
nime mpigia simu kaniambia kwamba walikuwa na masele kwenye hilo gari
lakini si kwamba amefariki hapana ila masele aligonga mtu akakamatwa na
raia wakavunja kioo na kutaka kumuua aligonga mtu wa kwanza na akataka
kukimbia akagonga mwingine ndio ilivyo kuwa lakini ni mzima na yupo
kituo cha police"