Waendaji wa club na sehemu za starehe hawatakuwa na wasiwasi tena
kuhusu simu zao kuishiwa chaji kutokana na kubuniwa kwa kaptura na
mabegi ya kulalia ambayo hutumia joto la mwili na muenendo (movement)
kuzalisha umeme.
Kaptura hizo zenye umeme zinaweza kuchajisha betri ya simu kwa kuvuna
nishati kutoka kwenye mwili wa binadamu kwa kutumia technojia ya
uzalishaji umeme kwa njia ya mwendo (kinetic energy) na thermoelectric.
Chaji hizo za kuvaliwa zimetengenezwa na kampuni ya simu ya Vodafone na chuo kikuu cha Southampton.