Wachezaji wawili wa Ivory Coast wametimuliwa kwenye kikosi kinachojiandaa na mchezo kuwania kufuzu michuano ya kombe la dunia mwaka 2014 dhidi ya Tanzania unaotarajiwa kupigwa uwanja wa Taifa siku ya Jumapili.
Mchezaji wa zamani wa Monaco Jean-Jacques Gosso Gosso, 30, ambaye kwa sasa anakipiga kwenye ligi ya Uturuki akiichezea Mersin na kinda la miaka 20 Abdul Razack wa Manchester City, ambaye kwa sasa yupo kwa mkopo Charlton Athletic, walipigana siku ya jumatano wakati timu yao ikiwa kwenye maandalizi ya mwisho kabla ya kuelekea Tanzania usiku wa leo.
FA ya Cote D’Ivoire imesema kwamba adhabu nyingine zinaweza kufuatiwa kutegemea na kamati ya nidhamu itakavyoamua