Search in This Blog

ZOEZI LA KUAGA MMWILI WA MAREHEMU MANGWEA LASITISHWA,MSAFARA KUELEKEA MOROGORO

Asakari Polisi wakitumia mbwa kutawanya maelefu ya watanzania waliotaka kuuaga mwili wa Mangwea baada ya muda uliopangwa kukamiliki. 








ZOEZI la kuuaga mwili wa aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya marehemu Albert Mangwea aliyefariki Dunia nchini Afrika Kusini Mei 28 umesitishwa huku umati mkubwa ukiwa haujamaliza kuuaga.

 
Kitendo cha Kamati ya maandalizi kukatisha zoezi la kuuaga mwili wa marehemu kwa sababu ya muda uliopangwa kukamilika iliwashangaza mamia ya watu waliok
uwa kwenye foleni ya kusubiri kupata nafasi ya kutoa heshma zao za mwisho mbele ya Jeneza la Mangwea.

Zoezi hilo liloanza saa 2:30 asubuhi imesitishwa saa 6:30 mchana kwa saa za Afrika Mashariki na Kati, na msafara ukiongozwa na Askari wa Jeshi la Polisi pamoja na vikosi vya ulinzi na usalama waliokuwa katika Viwanja vya Leaders Club.

Barabarani Asakari wa Kikoso Cha Usalama Barabarani pia walijiapanga vizuri kuhakikisha kwamba msafara wa mwili wa marehemu unapita vizuri katika maeneo yaliokuwa yamepangwa kuelekea mjini Morogoro.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Mr Blue alifika katika viwanja hivyo akiwa amechelewa na kukosa muda wa kuuaga mwili wa Mangwea lakini alipokutana na mashabiki wa muziki wake aliweza kusimama na kuwapa pole.

 
Mwili wa Mangwea hivi sasa uko safarini kuelekea Mjini Morogoro ambapo utalala nyumbani kwa mama yake na kesho uwakazi wa Mji huo pia watapata nafasi ya kutoa heshma zao za mwisho.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger