Hapa ni wakati Jokate alipoamua kukaa na Mpeka kistaarabu kuongea nae kabla ya hatua za kisheria
Msg alizotumia watu kwenye facebook na msg za simu za mkononi.
Aliefanikisha huyu jamaa kukamatwa ni mrembo mmoja model Blessing ambae
alishiriki Miss Morogoro 2013 ambapo namkariri akisema “wiki mbili zilizopita
nilipata msg kwamba Kidoti hair na Mzinga Planet wanahitaji mamodo kwa ajili ya
kutengeneza matangazo kwa ajili ya nywele za kidoti, tulikua Morogoro kwa ajili
ya Miss Morogoro tukaja Dar mpaka Mzalendo Pub msg ilipotuelekeza lakini
nilivyoingia sikuona mtu ambae anahusiana na Jokate, niliona watu ambao nawajua
lakini sio kuhusu nywele’
Endelea kusoma habari hii kwa kubofya hapa chini

‘Nikampigia
kaka mmoja anaitwa Johnson kwa sababu najua anafahamiana na Jokate, nikampigia
kumfokea kumwambia nyinyi vipi mbona mmetangaza audition alafu sioni hata mtu
mmoja ambae anahusika? naona watu ambao kampuni zao zipo majumbani kwao? baada
ya dakika zaidi ya 10 kina Jokate wakawa wameshafika japo baadhi ya mamodo
wengine walikua wameshaondoka lakini baadhi ya viongozi kama Majaji wa kike walikuepo
na walipoulizwa wakasema tumsubiri Mpeka ambae ndio muhusika na pia Mkurugenzi
wa Mzinga Planet” – Blessing
Baada ya
kina Jokate kufika Mpeka alipigiwa simu ili arudi Mzalendo Pub, japo alisita
sana mtuhumiwa huyu alikuja kwenye eneo la tukio na kukutana uso kwa uso na
Jokate na timu yake, baada ya hapo akaanza kusingizia kwamba yeye hausiki ila
kuna watu wengine ndio wanahusika ila alipotoa namba zao wakapigiwa simu, kila
mmoja alionekana kutaharuki kwa sababu hawajui chochote kuhusu hiyo Mzinga Planet.
Baada ya
Jokate na timu yake kukaa na Mpeka na kumuuliza kistaarabu bila kutoa
ushirikiano wa kutosha, uamuzi ulitoka kwamba apelekwe Polisi Osterbay ili
kuendelea na taratibu nyingine za kisheria.
Mpeka
alikua anaonekana analia wakati mwingie na hiyo ilikua ni baada ya kumpiga huyu
msichana shuhuda aitwae Blessing kwa sababu alimchomea mpaka akakamtwa.
HUU NDIO MWANZO WA KUWADAKA MATAPERI
WENGI WALIOKO FACEBOOK WAKIWATAPERI WATU KWA KUTUMIA MAJINA YA WATU
MAARUFU KAMA NA WEWE UNAHUSIKA KAA CHONJO

