ABIRIA WAKIPANDA KATIKA TRENI YA ABIRIA KATIKA STESHENI YA MOROGORO WAKATI WAKIELEKEA DAR ES SALAAM.
PICHA YA MAKTABA WWW.JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
.
LEO mnamo saa 11:30 asubuhi vichwa viwili vya treni ya huduma la
jiji la Dar es Salaam vilipata ajali ya kugongwa na roli la mizigo aina ya
Fusso katika makutano ya reli na barabara ya Kawawa jijini Dar es salaam ,
katika jali hiyo dereva wa Fusso alifariki duniani papohapo hata hivyo Utingo
wake alinusurika.
Hata hivyo vichwa hivyo vya treni vilipata mkosi tena wa ajali
ambapo viligongwa na basi dogo la Daladala aina ya Isuzu katika makutano ya
reli eneo la Kamata.
Tukio hilo lilisababisha majeruhi kadhaa katika basi hilo
la daladala ambapo majeruhi wamelaz
wa katika Hospitali ya Taifa Muhimbil
wakiwemo askari wawili Polisi kutoka Kikosi cha Reli mmojawapo
akiwa mahututi.
Vichwa hivyo viifanikiwa kufika stehesheni kwa wakati na kuanza
kutoa huduma ya usafiri wa treni jijini kutoka Dar Stesheni kwenda Ubungo
Maziwa hadi saa 5 asubuhi hata hivyo huduma ya leo jioni Julai 01, 2013,
imesogezwa mbele na itaanza saa 12 jioni badala ya saa 10:30 alasiri.
mabadiliko haya yamebidi yafanyike kufuatia Jiji la
Dar es Salaam kuwa na hekaheka ya kumpokea Raisi wa Marekani Barack Obama.
Aidha uongozi wa TRL unawataarifu wakazi wa jiji kuwa
kesho Julai 02, 2013, huduma za treni ya jiji hazitakuwepo hadi keshokutwa
Julai 03, 2013, ambapo zitaendelea kama kawaida.
Imtolewa na Afisi ya Uhusiano kwa Niaba ya Mkurugenzi Mtendaji
wa TRL,
Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu.
Makao Makuu ya TRL
Dar es Salaam.
Julai 01, 2013.