Lady Jaydee akiwa backstage na kiatu chake kilichosabisha ateleze jukwaani
Katika show hiyo Lady Jaydee alinunua kiatu cha rangi ya blue, kirefu
aka high heels chenye thamani ya shilingi 168,000. Yes laki moja na
elfu sitini na nane kama masikio yetu hayakutudanganya.
Hata hivyo urefu wa kiatu hicho ameutaja kuwa chanzo cha kuteleteza jukwaani kwenye show hiyo na kukaribia kumwangusha.
“Kuanguka jukwaani ni ajali kama ajali zingine, isitoshe sikuanguka
bali nilikaribia. Ila poleni kwa mlioumizwa na hicho kitendo…Nitapunguza
urefu wa viatu siku nyingine,” aliandika jana kwenye ukurasa wake wa
Facebook.
“Ni bahati mbaya tu, kwani hata Mwanza/Kahama/Dodoma vilikuwa virefu
kama hivyo hivyo na sikuteguka,” alitweet kufafanua kuhusu uvaaji wa
viatu virefu jukwaani