Japokuwa wahindi wamesusia kujihusisha tena na usambazaji wa albam za wasanii wa Bongo Flava, bado wanaufuatilia kwa ukaribu muziki huo.
Kupitia kipindi cha Power Jams cha East Africa Radio, mmoja wa wasambazaji wakubwa wa muziki Tanzania, Mamu, leo amewasifia Mwana FA na AY kwa hustle zao na jinsi wanavyotumia gharama kutengeneza video nzuri za baadhi ya ngoma zao na si kutegemea albam kama chanzo cha mapato yao ya muziki.
Hivi karibuni, FA na AY walishoot video ya wimbo wao Bila Kukuza Goti nchini Afrika Kusini.