Msanii
mwingine anaefanya vyema hivi sasa katika anga ya muziki wa
Bongofleva,Rich Mavoko akiwaimbisha mashabiki wake usiku huu,mbele ya
wakazi wa mji wa musoma waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la
Serengeti Fiesta 2013,ndani ya uwanja wa Karume mkoani Mara.
Madansa
wa msanii wa muziki wa kizazi kipya,Shilole wakitumbuiza jukwaani usiku
huu ndani ya Uwanja wa Karume,ndani ya mji wa Musoma mkoani Mara,ambapo
tamasha la serengeti fiesta 2013 likiendelea hivi sasa.
Anajiita
tajiri wa Mahaba Cassim Mganga kutoka Manzabay akiwaimbisha jukwaani
wakazi wa mji wa Musoma,wakati tamasha la serengeti fiesta 2013
likiendelea hivi sasa ndani ya uwanja wa Karume.
Mashabiki wakijinafasi kwa raha zao.
Kundi
la Wanaume TMK likiongozwa na Chege na Temba wakilishambulia jukwaa la
serengeti fiesta usiku huu ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani
Mara.
Mkali
mwingine wa muziki wa Reggae kutoka kanda ya Ziwa,Jita Man akiwakumusha
mashabiki wa muziki wake enzi hizo,mbele ya wakazi wa mji wa Musoma
usiku huu
Anaitwa
Godzilla kutoka maskani ya Sala sala,akishusha mistari yake live mbele
ya mashabiki wake waliojitokeza kwenye tamasha la serengeti fiesta usiku
huu.
Makamuzi yakiendelea jukwaani usiku huu.
Sehemu ya umati wa watu.
Msanii
wa muziki wa bongofleva ambaye kwa sasa anafanya vyema kwenye anga
hizo,Neylee akiimba jukwaani usiku huu wakati wa tamasha la serengeti
fiesta 2013 likiendelea usiku huu ndani ya uwanja wa Karume,Musoma
mkoani Mara.
Kundi
la Wanaume TMK Halisi likiongoza na msanii nguli Juna Nature
wakilishambulia vyema jukwaa usiku huu kwa staili yao mapanga shaa
shaa,huku mayowe yakipigwa kutoka mashabiki.
Kila shabiki alikuwa na mzuka wake.
Mashabiki wa tamasha la serengeti fiesta wakifuatilia yanayojiri ndani ya uwanja wa Karume hivi sasa
Sehemu ya umati wa watu ndani ya uwanja wa Karume usiku huu.
Mwanadada
Shilole akionesha umahiri wake wa kunengua jukwaani mbele ya maelfu ya
watazamaji waliojitokeza usiku huu kwenye tamasha la Serengeti fiesta
2013.
Anaitwa Linah Sanga,kutoka nyumba ya vipaji THT akiimba jukwaani usiku huu
Watu
kibao,kila mmoja akijaichai kivyake huku jukwaa likiwaka moto vilivyo
kwa miondoko ya bandika bandua ya wasanii wanaotumbuiza.
Wakali
wengine wanaokuja kwa kasi katika anga bongofleva-hip hop,Stamina na
Youngkiller wakilishambulia jukwaa kwa kushusha mistari mikavu live.
Shangwe kila kona za mashabiki zimetawala uwanjani hapa.