wanachama wa kundi la al-Qaida wanaohusishwa na shambulio la Westgate Mall la jijini Nairobi lililofanywa Jumamosi ya tarehe 21, Septemba 2013.
Mtu mmoja aliuawa bila mafanikio ya kumkamata mkusudiwa.
Mjini Washington, msemaji wa Pentagon bwana Gerger Little amethibitisha kuwa Marekani imehusika katika mapambano dhidi ya ugaidi (katika maeneo ambayo hakuyataja) na kufanikiwa kumkamata Mlibya kiongozi wa al-Qaeda katika nchi hiyo, Nazih Abdul-Hamed al-Ruqai anayefahamika pia kwa jina la Anas al-Libi (49)ambaye walikuwa wanamtafuta kwa udi na uvumba kwa kuhusishwa na shambulio la mwaka 1998 katika balozi za Marekani zilizopo nchini Kenya na Tanzania.
Ndugu wa al-Libi wamekaririwa wakiviambia vyombo vya habari kuwa ndugu yao alikamatwa siku Jumamosi nje ya nyumba yake huko mjini Tripoli mara tu alipokuwa akijiandaa kushuka kutoka garini.
Al-Libi ni mmoja wa watu waliokuwa wakitafutwa kwa dau la dola milioni $5 lililotolewa na FBI, kwa zaidi ya muongo mmoja.