UHUSIANO wa wasanii wawili wa filamu Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora’ na
Geofrey Kusila umeota mbawa baada ya kumwagana na kila mmoja kuendelea
na maisha yake.
Chanzo makini kilicho karibu na wasanii hao kimepenyeza habari kuwa uhusiano wao umevunjika bila kufahamika chanzo.
“Nora na Geofrey wameshaachana na kila mtu ana maisha yake hata kazi
hawafanyi tena pamoja, tangu walipoachana Nora anaandaa kipindi chake
cha kwenye runinga na hayupo tena na Geofrey,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, paparazi wetu alimtafuta Nora ili kuujua ukweli, akafunguka:
“Mimi ninafanya kazi zangu mwenyewe na Geofrey kivyake kwa sababu
tumeachana na kampuni ambayo tulikuwa ndiyo kwanza tumeianzisha nayo
imekufa na baada ya hapo kila mmoja akashika njia yake na kuangalia
jinsi gani atakavyofanya kazi hivyo hatupo pamoja tena.”