MKAZI wa Mtemwe, Unguja, Mashibu Suha (38), ambaye ni mvuvi amefariki baada ya kupigwa na radi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Englibert Kiondo, alisema tukio hilo lilitokea juzi, saa 6:00 mchana maeneo ya Magogoni ufukweni mwa bahari ya Hindi.
Alisema mtoa taarifa Ussi Mcha (38) mkazi wa Tungi ambaye pia ni mvuvi, alieleza kuwa akiwa maeneo hayo akiendesha ngarawa yenye jina la “Kila Mtu Ana Akili Yake”, alishuhudia tukio hilo.