Ni fedheha sana msibani!
MWIMBAJI maarufu wa nyimbo za Injili,
Bahati Bukuku hivi karibuni alipatwa na simanzi kubwa baada ya aliyekuwa
baba yake mdogo, Lwaga Bukuku kufariki dunia, lakini wakati kaburi
likiwa limechimbwa Sinza Makaburini, iliamriwa msiba huo usafirishwe
kwao Mbeya na hivyo kusababisha shimo hilo kuzikwa mgomba badala ya
mwili wa mtu.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea Novemba 7, mwaka huu, huko Tabata
Kisukuru wakati waombolezaji waliojitokeza kwa wingi wakiwa wanatoa
heshima za mwisho kwa marehemu ambaye alikuwa akazikwe kwenye Makaburi
ya Sinza, jijini Dar es Salaam ambako tayari kaburi lake lilishachimbwa.
Lwaga, baba mdogo wa mwimbaji huyo ambaye muda wote wa kuumwa kwake
alikuwa akiuguzwa naye, alifikwa na umauti Novemba 5, mwaka huu akiwa
Hospitali ya Kadinary inayomilikiwa na Dk. Mvungi iliyopo Ukonga jijini
Dar es Salaam na baada ya kifo chake, shughuli za msiba zilihamia
nyumbani kwa Bahati Tabata Kisukuru.
-gpl