Chanzo makini kilicho karibu na wasanii hao kilisema kuwa, Odama alikuwa na shughuli ya sendoff ya mdogo wake ambapo wasanii mbalimbali waliombwa michango lakini Shamsa hakutuma kwa wakati na kusababisha bifu kati yao.
Kilisema, zikiwa zimebaki siku tatu, alimtumia kwa njia ya mtandao elfu hamsini kitu ambacho hakikumfurahisha Odama na kuamua kumrudishia muda huohuo.
Shamsa Ford.
Chanzo kiliendelea kutiririka kuwa, baada ya Shamsa kuona
amerudishiwa fedha hizo, alimpigia simu Odama na kumuuliza kulikoni
lakini alijibiwa kuwa muda umekwisha hivyo hahitaji mchango wake tena.Baada ya kuzipata habari hizi, Weekly Star Exclusive ilizungumza na Shamsa ambapo alikiri kuwa ni kweli suala hilo lilitokea na kudai yeye hana tatizo na Odama.
“Niliona kawaida tu japo sikutegemea kama Odama angefanya hivyo kwa sababu ni msanii mwenzangu tunayefanya kazi kwa ukaribu sana japo nilichelewesha mchango na masharti yake yalikuwa hivyo kwamba ukichelewesha mchango hapokei,” alisema Shamsa.