Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiwafokea wafanyakazi wawili
wa kampuni ya Jiangxi Geo-Engineering (Group) Corporation kutoka China
baada ya kufumwa na msafara wake wakiiba mafuta ya Diesel kwenye tanki
la lori la la kumwagilia maji (Boza) la kampuni hiyo tarehe 19 Novemba
2013 Katika kijiji cha Ntendo Manispaa ya Sumbawanga.
Mkuu
huyo wa Mkoa alikemea tabia hiyo ya wafanyakazi wezi na kusema umekua
ni ugonjwa wa mda mrefu unaozorotesha kukamilika kwa ujenzi wa barabara
za lami zinazoendelea kujengwa Mkoani Rukwa.
Wafanyakazi hao waliokamatwa ni dereva William Ebron (kulia pichani)
na
kibarua Isaya Godwin ambao walifumwa majira ya saa nne asubuhi
wakinyonya mafuta kwenye tanki la Lori hilo lenye namba za usajili T-518
BDV mali ya kampuni hiyo kwa kutumia mpira wa kupitishia maji na
kumuwekea mteja kwenye dumu la lita tano, hata hivyo mteja huyo
alifanikiwa kukimbia.
Baada ya kuhojiwa walidai kuwa mteja wao huyo angelipia lita hizo tano kwa Tsh. 3500/= bei ambayo kihalali haiwezi kununua japo lita mbili za mafuta hayo katika soko.
Baada ya kuhojiwa walidai kuwa mteja wao huyo angelipia lita hizo tano kwa Tsh. 3500/= bei ambayo kihalali haiwezi kununua japo lita mbili za mafuta hayo katika soko.
Msafara
wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ulikua ukielekea katika kata ya Mtowisa kwa
ajili ya shughuli za kuhamasisha maendeleo ambapo ulikumbana na mkasa
huo njiani katika Kijiji cha Ntendo. Barabara ya Sumbawanga – Namayere
inajenga kwa kiwango cha lami na mkandarasi Jiangxi Geo-Engineering
(Group) Corporation kutoka China chini ya Mhandisi Mshauri Nicholas
O’Dwyer and Company Limited kutoka Ireland akishirikiana na Apex
Engineering Ltd. kutoka Tanzania kwa gharama ya Sh. bilioni 78.8 ambazo
ni fedha za ndani.
Watuhumiwa William Ebron (kulia) na kibarua Isaya Godwin (kushoto) muda mfupi baada ya fumanizi wakiwa hawana cha kujitetea.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiwakabidhi wezi hao kwa
vyombo vya usalama ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.
Mashuhuda wa tukio hilo.