Search in This Blog

TANESCO WATOA MAELEZO KWA KUANGUKA NGUZO SITA JIJINI DAR

Mafundi wa Tanesco wakiwa kazini.
Kufuatia tatizo la kugongwa na kuanguka kwa nguzo za msongo mkubwa zaidi ya tano katika Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, Afisa Uhusiano wa Tanesco, Badra Masoud amefunguka na kusema kuwa mafundi wapo kazini ambapo umeme utarejea kuanzia saa 1:00 usiku.
Akizungumza na mtandao huu muda mfupi uliopita, Badra alisema hadi muda huu polisi hawajanikiwa kuwakamata wahusika waliogonga nguzo moja na kusababisha nyingine kuanguka usiku wa kuamkia leo.
"Tatizo ni kubwa lakini mafundi wetu wapo kazini. tunatarajia hadi ifikapo saa moja usiku umeme utawaka maeneo yote yaliyoathirika hasa Kijitonyama," alisema Badra akiliomba jeshi la polisi kuwakamata haraka wahusika wa tatizo hilo.
Usiku wa kuamkia leo dereva asiyejulikana aligonga nguzo moja ya umeme jirani na Chuo Cha Posta Kijitonyama iliyoangusha nguzo zingine tano na kusababisha mlpuko mkubwa wa moto katika Barabara ya Ali Hassa Mwinyi maeneo ya Bamaga.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger