Gumzo kubwa kwenye harusi ya staa wa dunia katika Kundi la P-Square wanaotarajiwa kuangusha shoo Bongo
kesho, Peter Okoye mwishoni mwa wiki iliyopita, ni mwaliko wa msanii
pekee wa Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye alipondwa kwa
kuvaa suruali ‘njiwa’ (ya ajabuajabu).
Ishu hiyo ilijiri huko Lagos, Nigeria ilikofanyikia sherehe hiyo ambapo Peter alifunga ndoa ya kimila na mrembo wa haja, Lola Omotayo huku Diamond akipata fursa ya kukutana na baadhi ya mastaa wakubwa duniani, kasoro pekee ikawa kwenye mavazi.
Kwa
mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, Diamond alichemka kwa kuvaa
kivazi hicho kifupi miguuni kikiwa na mistari myeupe na myeusi hivyo
kusababisha kutukanwa mitandaoni.
WEMA, JOKATE KIVIPI?
Huku
wakitumia picha za waliowahi kuwa wapenzi wa Diamond, Wema Isaac Sepetu
na Jokate Mwegelo wakiwa wamevaa ‘taiti’ kama ‘kisuruali’ cha
mwanamuziki huyo, walieleza kuwa inawezekana wao ndiyo walimdizainia
hivyo kumsababishia matusi ya nguoni katika mitandao ya kijamii.
“Mafashenista wengi wanamtukana Diamond lakini inawezekana na zile
nguo kadizainiwa na Wema au Jokate kwa sababu ni staili zao. Nao wana
nguo kama hizo, hebu cheki kwenye picha,” alisema mmoja wa wachangiaji
wa mada hiyo katika mitandao ya Naija huku akitundika picha za Wema na
Jokate wakiwa wamevaa kama Diamond.
“Ni kweli Diamond amepata nafasi
kubwa ya kukutana na mastaa wakubwa na kutangaza muziki wake kimataifa
lakini kitu kimoja hakikwenda sawa.
“Ni juu ya nguo aliyokuwa ameivaa, mashabiki wengi wa muziki nchini
Nigeria walisema kachemka,” ilisomeka sehemu nyingine ya maoni ya
mashabiki wa muziki nchini humo.
Hata staa wa Nigeria aliyekuwa mmoja
wa wenyeji wa Diamond, Iyanya alipoposti picha akiwa na Diamond pamoja
na jamaa mwingine, ‘polisi jamii’ wa masuala ya mitindo waliendelea
kugongea msumari wa moto kuwa Diamond akubali kuwa kachemka.
STAILI YA MICHAEL JACKSON?
“Iyanya,
nani huyo kavaa suruali kama (marehemu) Michael Jackson? Mungu nisamehe
kwa kukutenda dhambi lakini ukweli hicho kivazi hakiendani na mwili
wake,” alifunguka shabiki mwingine kwenye ukurasa wa Iyanya wa
Instagram.
Mwingine alisema: “Najua amekopi kwa mtu wake anayemhusudu
(Wema), alionekana amependeza alipovaa hivyo walipokuwa China. Ukweli
(Diamond) hakupendeza au labda kachukulia kwa Jokate wa Kidoti?”
ANGEENDA KUBADILISHA
Baadhi
ya mashabiki hao walidai kuwa Diamond alipaswa kugundua kuwa yupo
tofauti na mastaa wengine ili arudi hotelini mara moja akabadilishe
nguo.
“Sijui alifikiria nini alipovaa hivyo, ona sasa amewaangusha na kuwadhalilisha mastaa wa Tanzania huko Afrika Magharibi.
“Ukweli ni kwamba kama alimuiga Wema na Jokate kachemsha, ona sasa wamemponza kwa kuvaa njiwa ya zebra kama wao.
“Diamond
anajua kuvaa sana lakini anapaswa kuwa na dizaina wa kumpa ushauri wa
mavazi kabla ya kwenda kwenye shughuli kubwa kama ile,” aliandika
Mtanzania aishie Nigeria.
KAPATA ‘KIKI’?
Katika
kujitetea huku akiamini kapata ‘kiki’ nchini Nigeria, Diamond alitumia
ukurasa wake wa Instagram kwa kutundika picha yake akiwa na kisuruali
hicho akiambatanisha na mastaa wakubwa wa Marekani kama akina Wiz
Khalifa wakiwa wamevaa njiwa kama yeye kuonesha kuwa ni fasheni ya
‘mbele’.
Hata hivyo, hiyo haikusaidia kwani mashabiki hao waliendelea
kumponda na kumtaka kujipanga zaidi siku akipata fursa kama hiyo kwani
mastaa aliojifananisha nao walivaa hivyo katika ‘iventi’ tofauti na
harusi.
MAMODO WANASEMAJE?
Ijumaa lilizungumza na baadhi ya mamodo maarufu wa Kibongo ambao walishuhudia vazi hilo ambapo walikuwa na haya ya kusema:
“Sijui
ni nani aliyemdizainia lakini kilichofanyika ni kwamba alimvalisha
Kimarekani, akasahau kuwa alitakiwa amvalishe Kiafrika au Kitanzania.
Unajua harusi yenyewe ilikuwa ya kimila haikutaka Umarekani hata kidogo
ndiyo maana watu walimponda Diamond. Naamini wakati mwingie
aliyemvalisha atafanya vizuri,” alisema modo maarufu wa Kiume Bongo,
Martin Kadinda.
“Unajua mitindo ya mavazi unaweza ukatulia,
ukadizaini kitu lakini ukifika mbele za watu wakakushangaa, hiyo ndiyo
fasheni ilivyo. Simlaumu Diamond wala sisemi alitakiwa ashone khanga au
kitenge lakini iwe changamoto kwa mamodo wetu waongeze ubunifu,” alisema
modo mwingine.
Pamoja na mambo mengine, safari ya Diamond nchini
humo ililenga kwenda kufanya kolabo na mastaa wawili wa Nigeria, Davido
na Iyanya.