Stori: Gladness Mallya
SEXY lady katika tasnia ya filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe amepata majanga baada ya gari lake kugonga gari lingine na vitu kibao kwenye siku ya ‘bethidei’ yake.
Habari zilieleza kuwa Wolper, badala ya kukanyaga breki alijikuta akikanyaga mafuta na kusababisha abomoe matenki ya maji na kupasua mabomba yote pia kugonga gari lingine lakini hakuumia ila presha ilishuka kidogo.
“Leo (Ijumaa) nilikuwa nauvaa ukuta ikiwa ndiyo kwanza naanza maandalizi ya kusherehekea bethidei yangu, nimebomoa matenki na nimepasua mabomba lakini yote namshukuru Mungu kwa kuwa sijaumia, asante Mungu wa wote kimbilio la wote na wewe ndiyo kimbilio langu, niombeeni jamani,” aliandika Wolper katika akaunti yake ya Instagram.