Kwa
miezi hii yote ilikua inajulikana Feza yupo Botswana kwa O’neal ambae
headlines zilitangaza sana kwamba mapenzi ya wawili hawa yanaweza
kuwafikisha mpaka kwenye ndoa.
Sasa
basi, mchapo wa leo ni kuhusu info mpya Exclusive on millardayo.com
kwamba Feza ameondoka Botswana na kuhamia South Africa ili kujijenga
zaidi kimuziki na pia kujitangaza na kuutangaza muziki wenyewe wa
bongofleva anaoufanya.
Swali la kwanza nililomuuliza baada ya kusema kahamia SA lilikua >>> Umehamia South Africa na boyfriend wako? akajibu ‘No, niko mwenyewe lakini na yeye kahamia sio mbali sana na hapa, ni majirani’
millardayo.com : Umehamishia makazi yako huko moja kwa moja? akajibu >>> ‘Hapana, nitakua part time huku na time nyingine Tanzania’
millardayo.com :
Na Boyfriend wako kahamia moja kwa moja South Africa? akajibu
>>> ‘Na yeye ana mazungumzo na Radio Stations za huku so
atahamia moja kwa moja, sijui zaidi ya hapo’
Credit:millardayo.com