Watu wanane wamekufa nchini Malawi wakati radi ilipopiga kanisa katika mji mkuu, Lilongwe.
Walioshuhudia wanasema kulitokea mtafaruku katika kanisa la Sabato baada ya jengo la kanisa kupigwa na radi Jumamosi jioni.Wakuu wa afya wanasema mtoto mmoja ni kati ya watu waliokufa.
Wameeleza kuwa watu 40 wengine wanatibiwa katika hospitali kuu.
Vyombo vya habari vya Malawi vinaripoti kuwa radi iliuwa watu watatu wengine katika matukio mbali-mbali tangu majira ya mvua kuanza mwezi uliopita.